Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Sidhani kama wanamtukana naona watu wana hasira mtoto mdogo anajaribu kuleta ubishi kwenye mambo yaliyowakuta watu.
Hasira ya nini badala ya kumfundisha? Hata mimi sijawahi kukutwa na uchawi wowote wala kuuona unadhani nitaamini?
Nitabisha tu maana sijawahi kuona kitu chochote cha kichawi kwenye maisha yangu.
 
Na hapa tunazungumzia uchawi wetu huu wa kiafrika.
Nilikuelewa tangu mwanzo ndio maana nikakasema labda ni uchawi wa kizungu (technology) ndo unaweza kuiba account.
Turudi kwenye uchawi wetu huu tunaoujua sisi...Acha kuchanganya mambo.
Mbon nmeshakueleza kila kitu mkuu au nimebakisha nini kingine,uchawi upo na utajiri wa wachawi sio pesa hizo elfu 10 elfu 5 tunazotumia mimi na wewe kwa hio wakiiba bank ni sawa na bure imani yao haiwaambii utajiri ni hayo makaratazi, nimekwambia uchawi ni imaani usikaze ubongo

Bado haujaelwa au bado ubongo umekakamaa?
 
Vizuri kabisa ila swala lililopo hapa ni_kwa lugha nyepesi "huwezi kukataa kitu usicho kijua na huwezi kukubali kitu usicho kijua" ishu ya hawa watu wengine "wanakataa wasivyo vijua na wanakubali wasivyo vijua" mpaka mtu anaenda kuokoka maana yake anakubali alikua dhambini hivyo anajikomboa, means anakataa anavyo vijua na anaenda kukubaliana na anavyo vijua, c dhani kama kuna mtu atakua anaenda kanisani huku ajui anachofuata au anaenda kanisani alafu ukimuuliza dhambi ninini akawa hajui dhambi ninini! Hivyo kwa dunia ya sasa kwa namna moja ama nyingine wengi ni waathirika wa matukio ya ulozi unaweza ukajua kua umedhurika pia unaweza usijue ila kua kuna mtu hajui kabisa kama kuna uchawi swala hilo na kataa! Binafsi sijawahi hudhuria ibada za kishetani yaani kwenda kwa mganga ama matambiko kulingana na mazingira niliyo kulia na malezi na nimesha pitia nyakati ngumu sana mpaka kufikia kutaka kushiriki ila nimeshwindwa, ila mbali na hyo yote naamini uchawi upo na kama usingekuwepo hivyo vilinge, nadharia za kichawi either muvi au story visinge kuwepo, unakutana na mtu anakuambia uchawi haupo alafu ni mlokole wakati humo humo kwenye biblia inamwambia " usimuache mwanamke mchawi akaishi " unaweza kuona huyu hata anacho kifuata huko kanisani hakijui zaidi ya kwenda ku socialize tu
 
Hasira ya nini badala ya kumfundisha? Hata mimi sijawahi kukutwa na uchawi wowote wala kuuona unadhani nitaamini?
Nitabisha tu maana sijawahi kuona kitu chochote cha kichawi kwenye maisha yangu.
Ni jambo la kufurahia na kuombea liwe hivyo maisha yote usisahau kinga ni bora kuliko tiba
 
Kumbe unajua kueleza vizuri sasa ukaleta mambo ya technology ukachanganya mambo.

Unasemaje utajiri wa kichawi ni pesa ndogo elf 10, 20 wakati tunaonyeshwa matajiri ambao mnasema wanatumia uchawi?
Watu wanapata utajiri kichawi. Iweje useme utajiri wa kichawi ni wa pesa ndogo.
 
Huyu nadhani hajawahi kurogwa mkuu siku akirogwa ndo atajua Nini maana ya urozi
 
Haa Mkuu
Nadhani Mleta Mada Hajui Kalyanda Juzi Imeondoka Na Kijiji

MBAYA Zaidi Wajinga Wapo Sehemu, Maeneo Mbalimbali Na Wenye Elimu Na Ujuzi Mbalimbali
 
Subil ukue w bado sana
 
Una moyo sana yani teeete! Teeete! Teeete! Uyooo! Mpaka atembee[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wamekusikia maana kuna mijitu hata tomaso alikua na nafuu
 
Na hapa tunazungumzia uchawi wetu huu wa kiafrika.
Nilikuelewa tangu mwanzo ndio maana nikakasema labda ni uchawi wa kizungu (technology) ndo unaweza kuiba account.
Turudi kwenye uchawi wetu huu tunaoujua sisi...Acha kuchanganya mambo.
Hakuna uchawi wa kizungu wala wa kikwetu uchawi ni uchawi tu shida ipo kwenye matumizi wenzetu wana u'transform nakua useful sisi tunaufanya unakua destractive hilo neno tech lisikuzuzue
 
Bado umekaza ubongo Demi
Nimesema kwamba wachawi utajiri wao sio pesa tunazotumia mimi na wewe, kwetu sisi mimi na wewe pesa ndio nguvu, ila utajiri wa wachawi upo katika nguvu za Imani yao sio haya makaratasi (fedha/pesa) kwao haya makaratasi sio chochote sio lolote ndio maana hauwakuti wameenda kukwapua bank na uchawi wa hivyo haupo maana Imani yao haiwaambii kua utajiri wao ni haya makaratasi,

Na pia umesema kwamba kuna watu wana utajiri wa kichawi narudia utajiri wa kichawi sio pesa unazozishika, yes wapo nakubariana nawe lakini sio wa kuiba bank ni wa kujishughulisha na kufanya kazi km binadamu wengine sio kufanya kazi kichawi,

Akihitaji kua na maendeleo lazima atajishughulisha ili apate pesa ila sio kwenda kuiba pesa bank kichawi

Na sio kwamba akiwa na pesa basi huo ndio utajiri wake hapana utajiri kwake km kweli yeye ni mchawi utajiri wake sio haya makaratasi
 
Kuwa mkristo hakukufanyi usiwe mjinga wa kuamini habari za wachawi kurushia watu magonjwa au majini kujificha chooni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…