Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Sawa saaasa kuhusu swala la insta haiibwi kwa kutumia uchawi wa kiimani ila ni uchawi wa technology,

Kwa hio nilikupa mfano wa kuibiwa a/c ya insta nikijaribu kukuonyesha jinsi inavyokua na matokeo yanavyokua linapokuja suala la uchawi,

Kuhusu kuiba bank haiwezekani kwa sababu, utajiri wa wachawi sio pesa hizi tunazozitumia mimi na wewe,

Ushaelewa au bado umekaza ubongo?
Akili za kuelewa wanazo na wanaelewa vzuri nachokiona wanachezea watu akili
 
Kumbe unajua kueleza vizuri sasa ukaleta mambo ya technology ukachanganya mambo.

Unasemaje utajiri wa kichawi ni pesa ndogo elf 10, 20 wakati tunaonyeshwa matajiri ambao mnasema wanatumia uchawi?
Watu wanapata utajiri kichawi. Iweje useme utajiri wa kichawi ni wa pesa ndogo.
Kupata utajiri kichawi hakuhusianishwi na kuiba elf kumi elf 20 kama chumaulete.
 
Tuko pamoja...
Okay Demi

Sasa, kwa kile ulichosema wewe kwamba mtu anaenda kuua mtu ili afanikiwe ni mchawi, hilo sijakubariana na wewe anaeenda kufanya jambo baya kwa minajiri ya kuwadhulu watu wengine basi huyo kwa namna moja au nyingine ni mshirikina hata km wataambatana na mchawi pamoja kwenda kufanya hilo jambo kwa pamoja watakachokifanya hapo sio uchawi bali ni ushirikina,

Emu ngoja nikufafanulie kidogo,

Uchawi mweupe, huu uchawi ufanywa kwa lengo la nia njema au kuombea mazuri au kuhitaji outcomes nzuri/njema zikutokee wewe au zimtokee mtu mwingine kwa kutumia portions na muunganiko wa mimea tiba/mizizi/magome ya miti ukiamini kwamba kuna jambo jema litatokea kwa Imani yako ya kichawi, usisahau kwamba uchawi ni Imani,

Kwa hio mchawi hufanya hivyo kwa kuamini jambo jema litatokea, mfano umempenda mtu fulani (kimapenzi) kwa wachawi hufanya uchawi mweupe wa kumpata mtu kimapenzi kichawi kwa kutumia uchawi mweupe, ingawa pia wapo wanaotumia uchawi mweusi (dark magic) kufanikisha jambo lao,

Sasa uchawi mweusi ni upi?

Niambie kwanza mpaka hapo umenielewa? Nataka twende taratibu sana ili nisije nikakuacha
 
Kwa wale wanaoamini uchawi upo wajibu maswali haya

1: uchawi ni nini

2: Nani anaemiliki huo uchawi na anaumiliki kwa namna gani

3: anauhamisha vipi kutoka kwenye umiliki wake na kuutuma kwenda kumdhuru kiumbe mwingine na unaingia kwa huyu kiumbe mwingine kupitia njia zipi.
"Kitabu kitakatifu biblia kimeandika usimuache mchawi aishi "
 
Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza. Nimekuja kugundua kuwa mambo mengi yanayoaminika kutokana na uchawi, yanaaminika hivyo sababu ya watu kuwa wajinga. Nitoe mifano.

1. Kuna mtu alikuwa anapata kinyesi cheusi. sasa sababu ya ujinga akawa anaamini amerogwa. Lakini kumbe kile kinyesi cheusi ni dalili ya vidonda vya tumbo, na ule weusi ni madini chuma kutoka kwenye damu inayomvuja tumboni.

2. Mtu mwingine akasema wazungu nao wachawi sana. kuna kijiji watu walikuwa wanakufa kwa radi. Mzungu akaja akasimamisha kamnara tu radi ikaacha kuua watu.

3. Wengi wanaamini vichaa wanaotembea barabarani wamerogwa. Lakini vichaa karibu vyote vinatokana na vichocheo kuyumba au kujeruhiwa kwa ubongo.

4. Watu wanaamini bundi wanatumiwa na wachawi sababu wanatembea usiku. Lakini tunajua uwezo wa bundi kuona usiku ndiyo unamuwezesha kufanya mawindo yake usiku.

5. Watu kwa ujinga wa kushindwa kupiga hesabu za mapato na matumizi, na kuweza kutunza pesa wanasingizia chuma ulete.

6. Magonjwa mengi hapo zamani yalidhaniwa kuwa yanatokana na kurogwa. Lakini sababu zake hasa zimekuja kufahamika. ujinga ndiyo ulifanya watu waamini kuna kurogwa. Kuna mchezaji amefariki juzi mguu unaoza yeye anasema ametupiwa jini.

7. Kanuni za kilimo zinajulikana lakini unakuta kuna watu wanaamini mtu anaweza kuroga apate mazao mengi, au akakuroga usipate mazao ya kutosha.

8.Madini yanapopatikana na jinsi ya kuyachimba huwa inafahamika, l;akini watu huwa wanaamini yanapatikana kwa uchawi.

9. Mara kuna uchawi wa kuleta mvua na hali habari ya ujio wa mvua na kutokuja zinajulikana.

10. Wengine wanaamini uchawi unaweza kukusaidia kwenye uvuvi.

11. wengine wanasema kuna wachawi huwa wanaingilia watu kingono!!1!

Kiufupi, wajinga wakishindwa kuelewa kitu wanasingizia uchawi. Hakuna kitu kinafunua ujinga wa mtu kama imani yake juu ya habari za kichawi. Jinsi ilivyo kali ndivyo ujinga wake ulivyo mkali zaidi.
Ona hili jinga
 
Okay Demi

Sasa, kwa kile ulichosema wewe kwamba mtu anaenda kuua mtu ili afanikiwe ni mchawi, hilo sijakubariana na wewe anaeenda kufanya jambo baya kwa minajiri ya kuwadhulu watu wengine basi huyo kwa namna moja au nyingine ni mshirikina hata km wataambatana na mchawi pamoja kwenda kufanya hilo jambo kwa pamoja watakachokifanya hapo sio uchawi bali ni ushirikina,

Emu ngoja nikufafanulie kidogo,

Uchawi mweupe, huu uchawi ufanywa kwa lengo la nia njema au kuombea mazuri au kuhitaji outcomes nzuri/njema zikutokee wewe au zimtokee mtu mwingine kwa kutumia portions na muunganiko wa mimea tiba/mizizi/magome ya miti ukiamini kwamba kuna jambo jema litatokea kwa Imani yako ya kichawi, usisahau kwamba uchawi ni Imani,

Kwa hio mchawi hufanya hivyo kwa kuamini jambo jema litatokea, mfano umempenda mtu fulani (kimapenzi) kwa wachawi hufanya uchawi mweupe wa kumpata mtu kimapenzi kichawi kwa kutumia uchawi mweupe, ingawa pia wapo wanaotumia uchawi mweusi (dark magic) kufanikisha jambo lao,

Sasa uchawi mweusi ni upi?

Niambie kwanza mpaka hapo umenielewa? Nataka twende taratibu sana ili nisije nikakuacha
Unaeleweka.
Kabla hujaenda mbali...tayari nimeelewa tofauti ya mchawi na mshirikina. Kwamba mshirikina anapata uwezo kutoka kwa mchawi. Hii ina maana ya kuwa mchawi anayo nguvu kubwa kuliko mshirikina.
Hii nguvu ya mchawi, je haina uwezo wa kuchukua pesa zote pale BOT?
 
Hiyo bank haijengwi tu kama watu wanavyojenga mabanda ya kuku.
Lazima uchawi na kafara vichukue nafasi.
Kwamba wachawi wanaoshiriki kwenye ujenzi wa Bank hakuna mchawi yoyote anayeweza kuwazidi...

Au hao wenyewe inakuaje wasiweze tena kurudi kuiba hizo pesa kiuchawi?
Kwamba hizo kafara wanazozifanya hakuna mchawi mwingine anayeweza kuzitengua?
 
Unaeleweka.
Kabla hujaenda mbali...tayari nimeelewa tofauti ya mchawi na mshirikina. Kwamba mshirikina anapata uwezo kutoka kwa mchawi. Hii ina maana ya kuwa mchawi anayo nguvu kubwa kuliko mshirikina.
Hii nguvu ya mchawi, je haina uwezo wa kuchukua pesa zote pale BOT?
Na kwa nn ukomae na kuchukua pesa BOT kwa nn usiulize kwa nn wachawi hawawezi kuingia ikulu na kuiba lile faili la njano na kutokomea nalo milele
 
Back
Top Bottom