Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Kuna siku nilipita na TAZARA hapo asubuhi (saa kumi na mbili) huku tumepewa mablanketi mazito, abiria mwenzangu ananiamsha, kuangalia nje vitoto vidogo vipo tumbo wazi! Hapo nikakumbuka ule msemo "binadamu anaishi kulingana na mazingira"!
Yeah hata mimi Njombe wakati naishi nilizoea na nikawa naoga maji yale ya baridi kabisa na fresh ,navaa Vest fresh ila Makete sikuwahi kuwaza huo upuuzi kule ilikua zaidi ya hatari
 
Afu baridi Ina impact gani kwenye kimo Cha watu maana nyanda za juu kusini kukutana na watu warefu ni nadra sana

Sijajua hata upande wa uchaggani maeneo yenye baridi Kali kama kule Rombo wengi wanakimo kifupi.

Upareni nako vivyohivyo maeneo yenye baridi ya upareni wàfupi NI wengi kuliko warefu,

Ukienda Uluguruni vivyohivyo, wakazi wa milimani kwèñye baridi NI wàfupi kuliko wanaozaa maeneo yenye unafuu wa Hali ya hewa, ûkienda Turiani kule kibati utaona wafupi niwengi kuliko warefu, nenda kisaki, Mvuha Mpaka matombo nako halikadhalika.
 
Sehemu za baridi kama unaona mwili unakataa ni kheri ukakimbia mapema.

Waliokulia maeneo ya pwani wakienda hata kwa mara moja huwa hawatamani kurudi.

Mwezi wa 6 na 7 ndo naona kuna kijibaridi dar, ambacho walau mtu anajifunika shuka asubuhi.

Wakati baadhi ya maeneo huko iringa, njombe au mbeya hata mchana tu ni lazima uvae koti zito kwa baridi lake.
 
Bahati mbaya ilikuwa ni siku yangu ya kwanza sikubeba hata sweta nilikuwa natetemeka kama kinda la ndege

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
Mjifunze hata kujua miezi ya baridi hapa Tanzania ili ubebe hata makoto. Kuanzi June-August hunipeleki Makambako Njombe,Makete Lushoto na sehemu yoyote inayosifika kwa baridi hapa Tz.
 
1. Tembea duniani ukutane na baridi. Ya Mafinga cha mtoto.

2. Niliwahi kuishi Lesotho baridi mpaka Maji kwenye mabomba yanaganda. Mabomba hayatoi maji huko bila heater ndani haulali.
Miaka ya 90 nikiwa nronga - machame kuna kampuni moja ya msaada kama sikosei ni DANIDA ilisambaza maji kwa kutumia mabomba ya chuma.

Maji yale yalikuwa yanavunwa mlimani klm waliweka ma tank huko juu hivyo yanashuka yenyewe bila hata pump.

Shida ilikuwa kutokana na baridi maji yapo lkn hayatoki maana ni barafu tu limeganda ndani.

Pamoja na kubadilisha kuweka ya plastiki lkn zoezi lilifanikiwa kwa asilimia 40 nafuu kidogo kuliko mwanzo.

Tangu niondoke kule nronga miaka hiyo hiyo ya 90's sijawahi kurudi tena.
 
Back
Top Bottom