Hali ilivyo kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Hali ilivyo kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Picha za hali ya kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya jana Jumatano Septemba 11, 2024 kuvamiwa na wananchi huku wakifanya uharibifu wa baadhi ya mali ikiwamo gari.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa yake jana Jumatano kuhusu tukio hilo, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania ni wezi wa watoto kisha kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela baada ya watu hao kwenye gari, akawapeleka kituoni, hata hivyo wananchi takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amedai Misime.

Amesema licha ya askari polisi kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa kujichukulia sheria mkononi, wananchi hao walikaidi na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua watu hao wawili kwa nguvu ili wawaue.
Snapinsta.app_459443619_1242060363472737_8890806217596749107_n_1080.jpg
Snapinsta.app_459255706_886092856467533_8675677239033746008_n_1080.jpg
 
Safi sana.
Unapongeza uhalifu na ujinga?
Kuna uhakika gani hao watu wawili ni wezi wa watoto?
Kuna watu wameshauwawa Dodoma kimakosa sababu ya jambo kama hili.
Kuna gari kadhaa zimesha chomwa Moto kwa mambo ya kuhisia wezi wa watoto.
Subiri yakimtokea nduguyo au wewe mwenyewe utaona ubaya wa kufanya hivyo.
 
U

Unapongeza uhalifu na ujinga?
Kuna uhakika gani hao watu wawili wezi wa watoto?
Kuna watu wameshauwawa Dodoma kwa kimakosa sababu ya jambo kama hili.
Kuna gari kadhaa zimesha chomwa Moto kwa mambo ya kuhisia wezi wa watoto.
Subiri yakimtokea nduguyo au wewe mwenyewe utaona ubaya wa kufanya hivyo.
Tulia watu watoe ya moyoni
 
Ukombozi utaletwa na watu wa mikoani.siyo watu wa dar es salaam mtu anatekwa mchana kweupe anashushwa kwenye gari wanaangalia tu.ingekuwa kwetu Huku mikoani hizo gari za watekaji zingekuwa majivu kabla ya kumwingiza kwenye gari zao waliyemteka
 
Back
Top Bottom