Hali ilivyo kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Hali ilivyo kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Viongozi wetu waone aibu Kwa Kweli hivi hawajifunzagi au hata kuona wivu Kwa mazingira safii na miundombinu kiujumla Kwa hao wenzetu huko wanakoendaga kuchukua mikopo,,,Sasa Kwa Mazingira hayo ndio ofisi,,,nyumba zao Je??Wanajithamini sana wao kwa kujilipa maposho makubwa,,,vijana wao hoi kiafya na kimazingira,,,wataacha kula rushwa na kufanya vitu vya hovyo?? Sidhani!
 
Unapongeza uhalifu na ujinga?
Kuna uhakika gani hao watu wawili ni wezi wa watoto?
Kuna watu wameshauwawa Dodoma kimakosa sababu ya jambo kama hili.
Kuna gari kadhaa zimesha chomwa Moto kwa mambo ya kuhisia wezi wa watoto.
Subiri yakimtokea nduguyo au wewe mwenyewe utaona ubaya wa kufanya hivyo.
Sijawaza huko
Mimi numefurahi kupondwa mawe hicho kituo na hiyo gali, ccm wajenge kipya
Halleluya
 
Dalili ya mvua ni mawingu.
Hii inaonyesha tayari wananchi washaanza kuchoshwa na mambo mbalimbali, na unaweza kuta hapo ni kiaingizio tu kumbe wana mengi mioyoni mwao.
Hayo yaliyo moyoni mwao wataenda kuyatolea jela. Yaani msako utakaopita kwenye hicho kijiji watahadithia vizazi vyao vyote.
 

Picha za hali ya kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya jana Jumatano Septemba 11, 2024 kuvamiwa na wananchi huku wakifanya uharibifu wa baadhi ya mali ikiwamo gari.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa yake jana Jumatano kuhusu tukio hilo, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania ni wezi wa watoto kisha kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela baada ya watu hao kwenye gari, akawapeleka kituoni, hata hivyo wananchi takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amedai Misime.

Amesema licha ya askari polisi kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa kujichukulia sheria mkononi, wananchi hao walikaidi na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua watu hao wawili kwa nguvu ili wawaue.
View attachment 3093941View attachment 3093948
Mwanachi co.tz ndio gazeti pekee lililobaki ambalo angalao linatoa taarifa zenye kuaminika.
 
Back
Top Bottom