Hali ilivyo kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Picha za hali ya kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya jana Jumatano Septemba 11, 2024 kuvamiwa na wananchi huku wakifanya uharibifu wa baadhi ya mali ikiwamo gari.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa yake jana Jumatano kuhusu tukio hilo, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania ni wezi wa watoto kisha kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela baada ya watu hao kwenye gari, akawapeleka kituoni, hata hivyo wananchi takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amedai Misime.

Amesema licha ya askari polisi kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa kujichukulia sheria mkononi, wananchi hao walikaidi na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua watu hao wawili kwa nguvu ili wawaue.
View attachment 3093941View attachment 3093948
Naunga mkono hoja
 
Wananchi wamekosa imani na vyombo vya dola.na mahakama.

Sheria mkononi
 
Kwahio hadi polisi hawajathibitisha kuwa hao watoto walitekwa au la, Ila wamekomaa na wananchi walioamua kujilinda wenyewe baada ya watu waliopewa dhamana kufanya tofauti
Mtoto mmoja alikuwa kabebwa na baba yake na mwengine ni wa kaka wa mama wa huyo mtoto. Kwa kifupi wasukuma walitaka kuwaua wazazi wa hao watoto.
 
Back
Top Bottom