DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hili jambo ni la jamii nzima, sio kwamba sisi ni kikundi Cha watu flani maalumu kilichotengwa hapana!! Sisi wote hapa Tuna ndugu, jamaa na marafiki.. haipendezi wakiwa wamesoma halafu wabaki kuwa tegemezi!!

Hii ni jamii yenu ambayo mnatakiwa mpaze sauti kwaajili yake!! Nna watu nawafahamu wengi wao Wana miaka 5, 7 na mpaka 10 hawajapata ajira ya kabisa tangu wamalize vyuo vikuu na Wanasumbuka kweny Hali zao za kuwa Walemavu.

Wengi wanasema wamefika mpka wizarani wanapohusika na Ajira, vijana na watu wenye ulemavu. Wanaishia kuandikwa majina na kupewa ahadi hewa!

Miaka inapita, umri unaenda, na Hali ya kukata tamaa inatuandama
 
Hata mtu anaposomea anaangalia kazi ambayo anaimudu kulingana na madhaifu yake!!. . Kwahio wote wanao apply kazi maana ake wanaijua kazi Yao na wameisomea
Taja mfano wa kazi unayoimudu
 
Watanzania wengi hawathamini walemavu.

Kuna mtu kaweka video ya nyumba anayoipenda.

Nyumba mbele ina mingazingazi kibao.

Nikamwambia hapo mbele panatakiwa kuwa na sehemu isiyo na ngazi, iwe na flat slope. Kwa watu wanaotumia wheelchair.
.
Watu hawafikirii hayo.

Rais wa nchi alihoji kwa nini hospitali ya serikali ina lift. Aliona ni anasa.

Hakuelewa kabisa pale ni hospitali wanakuja watu wa kuka aina, wagonjwa, walemavu etc.

Huyo rais, alikuwa na PhD.

Hatujali.
 
Pole sana, ila mwenyewe ulisema ni bonge la pisi mpaka Makumbusho walikushangaa so kawaida hiyo!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka, sijawahi sema hivyo. Na uzi haukuwa unahusu u pisi.
 
nimecheka, sijawahi sema hivyo. Na uzi haukuwa unahusu u pisi.
Ogopa teknolojia!


kuna mtu aliwahi nambia ukienda makumbusho utajikuta unakodolea macho watu, hiyo siku nkawaka na kusepea hapo maeneo, cha ajabu wao wakawa wananikodolea mie macho, afu cna habariii.


 
Tuwaelewe vipi! Mbele ya wanasiasa mnasema mnapewa nafasi sawa na mnashangilia hotuba zao, huku mnafai hampewi fursa sawa na raia wengine! Siku zote mimi husema usijaribu kumtetea mtanzania atakudodoshea zigo.
 
Taja mfano wa kazi unayoimudu
Mi nimesomea Bachelor of Business Administration in Finance... Ndo hapo napofanyia kazi! Lakn nna uwezo wa kucop na idea mpya ya kazi hata Kama haipo kweny eneo hilo
 
Tusaidieni kupaza saut, kweny ujenzi pia ni muhimu kuzingatia Hilo.. haipendezi mtu kubebwa bebwa,
 
Wewe unafikiri mwaka huu unaweza kupitia bila kuwa mlemavu? Mungu na aichukue miguu aliyokupa utembelee makalio.
Ni maoni yake, japo si vizuri ku generalize kwa wote! Ibakie kuwa ni character za kibinadamu tu
 
Tuwaelewe vipi! Mbele ya wanasiasa mnasema mnapewa nafasi sawa na mnashangilia hotuba zao, huku mnafai hampewi fursa sawa na raia wengine! Siku zote mimi husema usijaribu kumtetea mtanzania atakudodoshea zigo.
Najua unajua Hali halisi ya maisha ya kitanzania!! Japo sijawahi kushuhudia Hilo lakn sikumbuki Kama nimewahi kuitwa kikao chochote kwaajili ya hio ajenda
 
So sorry,
Nimetoa Machozi ,Nimelia Kiukweli..
Kuna Hizi Ajira za TRA wametoa Juzi kati hebu jaribu Kuomba Kama Una Degree ya Usimamizi wa Fedha..
 

Attachments

Pole sana mkuu
Pia humu kuna wadau ungeweka profile yako hapa huenda ungeweza kuonekana ukapata fursa
 
Pole sana mkuu
Pia humu kuna wadau ungeweka profile yako hapa huenda ungeweza kuonekana ukapata fursa
Ni kweli kabisa kiongozi, japo natamn na wengine wasaidike pia! Natamn serikali itafute mfumo maalumu wa ku recruit graduate wote weny matatizo ya viungo ili kuwapunguzia ukali wa maisha!!

Mtu atakaye hitaji nimpe profile yangu!! ili angalau anikwamue ntakua tayari kumtumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…