Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Uchaguzi 2020 Hali si shwari ndani ya CCM, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally amekemea vikali baadhi ya wanachama wanaopanga kukisaliti chama

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Bashiru Ally Kakurwa amekemea vikali tabia za baadhi ya wanachama wa CCM wanaopanga kukisaliti Chama katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu kwa maslahi yao binafsi. Ameahidi kuwachukulia hatua kali watakaobainika kusaliti Chama ikiwemo kuwafukuza Uanachama...
Kakurwa upandacho ndicho uvunacho. Tuliwakaribisha wapinzani ndani ya chama na kuwapa vyeo,kama kina kina Kitila Mkumbo.
Sasa watu wanaona heri wachague tu watu wawapendao, kukishabikia chama kibinafsi hakulipi.
 
Wote walio kwenye nafasi kubwa za uongozi wa CCM hawana moyo na chama kwa vile nao ni watu wa kuja kutafuta masilahi.

Bashiru Ally Kakurwa ni CUF damu, Humphrey Pole Pole ni CHADEMA na Magufuli ni NCCR. Na wale wenye chama wamenyang'anywa na wanadharaulika sana.

Najuwa kura ni siri ya mtu lakini sioni wafuatao wakiipiga CCM kura za U-Rais; Kikwete, Mama Maria Nyerere, Makongoro, Butiku, Msekwa, Makamba Sr, Makamba Jr, Nnape na Kinana.

Hao ni mfano tu lakini ni wengi sana CCM imebakia usoni, rohoni ni CHADEMA au Opposition.
 
Bashiru Katibu Mkuu wa Ccm aneishaufyata huko anahaaha na kusema kuwa Ccm watapiga kura Kwa upinzani na kusema kuwa atawashughulikia na kuwafukuza, Kwan atawajuaje Wakati kura ni Siri?

Sasa atawashughulikiaje Wakati chama kitakuwa kimeishakura mweleka? Ubabe utakuwa umekoma? Nani kakuambia kuwa nguvu husaidia?
 
Mama Samia suluhu kachokoza nyuki tunduni...kapokea waunga juhudi wapya ...kituko ni pale hao wanachama wapya waliovutiwa sana na sera na ilani ya ccm wote wanatoka CHADEMA..
Wewe mwenyewe mpiga debe tu, kule saccos yawezekana hata kadi huna.
 
Mwambie Bashiru asitutishe! Nani aliwaambia wafanye ubabe na kutuona wanaCCM ni wajinga? Inakuwaje tunachagua watu wanawakata? Inakuwaje wanachapisha fomu moja ya uraisi na kuzuia watu wasigombee uraisi?

Mwambie pia wanaCCM tuna uhuru kama wananchi wa Tanzania wa kumuunga mgombea urais, ubunge na udiwani wa Chama chochote kile na wala sio dhambi.
Kwani watajuaje nani kamchagua nani? Kura ni siri! Kila mtu awe huru kumchagua anaemtaka
 
Wewe mwenyewe mpiga debe tu, kule saccos yawezekana hata kadi huna.
Uchaguzi wa mwaka huu hata kama unakadi na imani wengi bado hawajajua wampigie nani. Mpaka tarehe 28.10 lolote linaweza kutokea maamuzi ni wakati wowote....
 
Back
Top Bottom