Hali tete Simiyu, wananchi wanalazimishwa kwenda kwenye ziara ya Rais Samia

Hali tete Simiyu, wananchi wanalazimishwa kwenda kwenye ziara ya Rais Samia

Kimsingi hakuna mgeni wa mambo haya kwa sasa nchini na wasiwasi ni ule ule wa kushindwa, ila usisahau bismillah haimpunguzii kuku maumivu ya kisu ...so we waangalie tu na drama zake ila bakora ziko pale pale Oktoba, No reform No election
 
Hali ni tete hapa mkoani Simiyu. Raisi Samia atakuwa na ziara hapa.

Sasa maandalizi ya kuonyesha kuwa anakubalika yamekuwa ni maumivu Kwa raia.

Raisi atakapo pita wafanya bihashara wameamliwa kufunga maduka, watumishi wote,Sungusungu ,Mgambo wameamliwa kuhudhuria mikutano ya Samia.

Wenye shule za English medium wameamliwa kutoa magari ya Shule Kwa ajiri ya kusomba raia.

Je hii nguvu kubwa ya Nini, je serikali ya mkoa inawasiwasi kuwa wananchi wanaweza susia mikutano ya Raisi?

Tuombeeni sisi wana Simiyu maana maagizo ni mengi
Wazushi kama nyie mnatakiwa kushughulikiwa.

Rais hawezi lazimisha mtu Utaenda mwenyewe tuu kwani wewe hupendi Kumuona Rais na msafara wake?
 
Dk za mwisho ndio ana fanya ziara vijijini nazani hapendi ila ni kasukumwa tu kama jinga
 
OGOPA SANA.
Hii TK Movement ni nani?

Yaani tayari hawa watu wameanza "Kumpigia Kura Samia", hata kabla ya siku ya uchaguzi/uchafuzi?

Nani atakubali upumbavu huu!

Maana ya fomu hiyo ni kwamba, wanachama wote wa CCM (wanaodaiwa kufikia 13 milioni), tayari watakuwa wamemchagua Samia Suluhu Hassan bila ya hiari yao. Walimu wote na watumishi wa serikali watalazimishwa kujaza fomu hiyo, na kuhakikisha wanahimizwa siku ya uchaguzi kujitokeza kwenye kituo cha kupigia kura.
Hivyo hivyo na wengine, watapelekewa vitisho au hata rushwa; kwani taarifa zao tayari hao TK Movement wanazo.

Huu ni ujambazi!
 
Huu ni upotoshaji. Mahali popote atakapotembelea Mh Rais , maelfu ya wananchi huwa na shauku ya kwenda kumuona
security system ya rais ni tightlly utamuonaje rais kirahisi kama zamani? Utaishia kumuona kwenye screen zilizofungwa uwanjani, tena mpaka uingie ndani ya uzio mzito wenye ulinzi mkali na ukaguzi wa hali ya juu kana kwamba umebeba vitu vya hatari. Huo ukaguzi ni kama udhalilishaji tu! Ya nini kwenda kudhalilika uwanjani kumuona rais? Bora ubaki nyumbani utaangalia tv bila kero. Zamani marais tuliwaona kwa karibu kwa jinsi tulivyoweza kupenya na kufika karibu na jukwa lake. Sasa hivi jukwaa lake limetengwa mbali humuoni vema raisi bila msaada wa screen za uwanjani.
 
Back
Top Bottom