Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Kuna siku aliingia kitambaa cheupe Ile Tabata akawanyang'anya pombe Na kuwagawia marafiki zake anaowafahamu yeye Na kuondoka zake......ukweli ni kuwa chidbenz hashauliki....
 
Kutoa tuu taarifa inaweza ikawa msaada coz JF ni platform kubwa sana, angalia hii thread sahv ina views zaidi 5k, utajuaje mmoja kati yao akafanya maamuzi ya kwenda kumsaidia?
Hata kama ingekua na views milioni mia,hiyo haikupi uhakika kua Chid amepata msaad,ila msaada wako kwake ingekua ni uhakika,

Wewe hukua na uwezo wa kumsaidia? kwanini unawalaumu wasanii kutomsaidia? unaonaje ukaanza kujilaumu wewe kwanza? Be the change that u want to see in the World,usitegemee wengine wafanya kwa ajili yako.
 
Walikuwa hawana utaalamu wa huduma ya kwanza.......Hayo ni makosa yake mwenyewe sio masela mavi sijui upumbavu gani, mtu umelewa unashauriwa usiende kuogelea, unalazimisha, unazama unakufa
Wanachoweza kufanya watu ni kukushauri, ila ukishauriwa ukapuuza ni juu yako, hao sio mama zako...
 
Amsaidie kwani yule ni mtoto wake? Hakuna mtu anayewajibika kwa maisha ya mtu mzima mwenzake mzee
 
Amsaidie kwani yule ni mtoto wake? Hakuna mtu anayewajibika kwa maisha ya mtu mzima mwenzake mzee
Kwahiyo lengo la huu uzi wake lilikua ni nini? au huu uzi umewalenga wazazi wa Chid ili wamsaidie? wao hawajui hali aliyonayo mtoto wao?
 
madawa atumie yeye kuumia uumie wewe..chid alikua miyeyusho utoto wa mjini mwingi
hasaidiki. dk 2 mbele anakuchenjia. yeye aishi tu akifa tunazika. ndio maisha.
 
Mkuu Chidibenz angekua kaka ako ,sidhani kama ungemuacha aendelee kuishi maisha anayoishi sasa
Mkuu,

Hata angekuwa kaka yako, usingekua na cha kufanya, trust me.

Chid ameanza madawa arround 2010. Ni miaka 15 karibu sasa ndugu, jamaa, marafiki, wasanii, na kila aliekua na nafasi ya kujaribu kumsaidia wamejaribu, na imeshindikana. Hapo alipofikia naamini hata mama yake mwenyewe hataki kumsikia, achilia mbali kumuona. Ndio maana wamemuacha, aishi maisha aliyoyachagua mpaka hapo atakapoishia.

Kama umewahi kuwa na mtu wa aina hii kwenye familia yenu, utanielewa.
 
Siku zote binadamu huwa tunavuna tulichopanda, Chidi Benz kitakachomsaidia kubadilika ni yeye mwenyewe kuamuakuwa anatakiwa kubadilika na niwajibu wake na siyo watu au sisi mashabiki tumsaidie kubadilika maana ni mtu mzima. Kingine aache kudeka na kujiona yeye si mtu special anaehitaji huruma, dunia haipo hivyo. Ila kwa wengine ambao tunaona mbali tatizo kubwa la Chidi limeanza kwenye familia na tatizo hilo "Fatherlessness" , mkubalinau mkatae Baba ninkiungo muhimu sanaa kwenye malezi ya mtoto wa kiume.
 
Mkuu Chidibenz angekua kaka ako ,sidhani kama ungemuacha aendelee kuishi maisha anayoishi sasa
Mkuu usichojua ni kwamba kina chidi benz tunaishi nao hata huku mtaani kwetu, ndugu zetu, watoto wetu, marafiki zetu. Nimesema hivyo kwa sababu nimeshawahi ishi na ndugu mwenye changamoto kama ya chidi, sio kwamba hatuwajali ila kuna muda hawasaidiki kutokana na hali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…