Hali ya maisha imekuwa tete sana. Mawaziri mnakula vizuri, sisi hali mbaya

NI AIBU KWA MTANZANIA KULALAMIKIA VITU KAMA,
Mchele
Maharagwe.
Mafuta.
Unga
AMBAVYO VINALIMWA HAPAHAPA TZ...
Mpo mijini mnazurulazulura na mikeka mikononi mmeacha maeneo ya kulimia wanachungia ngo'mbe tu, halafu daily kulalamika bei ya unga wa ugali serious! Haya njoo uchukue debe mbili za mahindi ukasage unga
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Kweli kiongozi, watu wanazurura na mikeka, soksi na boxa kwenye baa na maeneo mbalimbali huko alafu anataka ale kwa bei rahisi. Maisha hayarudi nyuma usiombe yakuache utajuta milele
 
Kamwe maisha hayamsubiri mvivu na mjinga. Pambana uende nayo sambamba. Bidhaa hazijawahi kuwa bei nafuu kwa mtu asiyejituma na kutumia akili
 
Hao uliowataja unataka wakakulimie au? Hii tabia ya utegemezi na kudhani watu Fulani ndio wekusababishia Ugumu wa Maisha ni mbaya sana.
Kimfano garama za huduma za afya nazo tukalime? Bei za mafuta, na tozo!

Kumbuka ktk ripoti ya c.a.g. wamekwapua mabilion kadhaa na hujuma kibao, hayo na madudu mengine ndio yanazidisha ugumu wa maisha kwa wa tz.

Serekali ina wajibu wa kuboresha maisha ya raia wake.
 

Hata yule mataafu anayeangusha birthday parties NY ana mawazo kama wewe.

Vipi nawe ni mhuni, mlamba asali au kijana hovyo hovyo tu?
 
Kwa hiyo hao uliowataja ndio wanesababisha gharama za Afya kuwa Juu?
CAG ametaja jina la mtu kwenye ripoti yake?
 
Hata yule mataafu anayeangusha birthday parties NY ana mawazo kama wewe.

Vipi nawe ni mhuni, mlamba asali au kijana hovyo hovyo tu?
Rudi kijjn ukalime mkuu, mvua zote hizo ww umejificha kwenye kibanda Cha kubetia unasikilizia ushinde mil. 200😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…