Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Ndivyo ilivyo mkuu.
Toa ulicho na uwezo nacho, sio unatoa unabaki na manung'uniko na kuanza msimulia kila mtu ali ulimsaidia fulani
Daaha mkuu yaani kuna kipindi hadi nikawa nasema au shida nimelogwa.

Ila nikagundua hapana ni vile show kali tuu
 
Wasalam.
Ndugu jamaa na marafiki.
Hali ya mjini hapa dasalama ni tofauti na nilivofikilia nimeamini mjini pazito 🙌🙌🙌🙌.

Mjini pazito aiseee. yaani nilijua nikishapata biasahara ndo nishamaliza kumbe bado kuna kusugua sana.

Mjini pazito nyie watu hawana huruma kabisa. Bora ningebaki mkoani huko.

Ila ngoja nikaze hivi hivi mpaka kieleweke kikubwa tunapata cha halali....

Kuna time unapitia hata hamu za wanawake unakua huna kabisa kutokana na ugumu wa life hapa dasalamu.

Mjini pazito 🙌 🙌 🙌 🙌
Pengine maneno ya chidbenzi yana ukwel, iyo mbuga nzito
 
Hiyo siyo" typing error", "typo" zinafahamika na ujinga unafahamika.

Mtu anaeshindwa kutofautisha hata R na L ni lazima mjini apaone "pazito".

Yote ipo kichwani kwa mtu.

Fikiria sisi tuliozaliwa na kukulia mjini utwambie mjini "pazito", tutakuelewa kweli?

Uzit na wepesi wa maisha upo mawazoni mwetu, siyo uhalisia.

"pazito" pana kilo ngapi na huko kwepesi pana kilo ngapi?
Naunga mkono hoja hii maza, matanzania mengi hayajui tofauti ya R na L, penye R wanaweka L, penye L inapachikwa R. Hii ni mpaka kwa wale wanaojiita wasomi, inatia kichefuchefu sana
 
Naunga mkono hoja hii maza, matanzania mengi hayajui tofauti ya R na L, penye R wanaweka L, penye L inapachikwa R. Hii ni mpaka kwa wale wanaojiita wasomi, inatia kichefuchefu sana
Ili uwe msomu inabidi uwe na vigezo gani.
Ukute mnaunga mkono kumkandamiza mtu ambaye sio msomi..
Badala ya kuelekeza nyie mnakalia kukosoa
 
Back
Top Bottom