Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Wasalam Ndugu jamaa na marafiki.

Hali ya mjini hapa Dasalama ni tofauti na nilivofikiria nimeamini mjini pazito 🙌🙌🙌🙌.

Mjini pazito aiseee. yaani nilijua nikishapata biashara ndio nishamaliza kumbe bado kuna kusugua sana.

Mjini pazito nyie watu hawana huruma kabisa. Bora ningebaki mkoani huko.

Ila ngoja nikaze hivi hivi mpaka kieleweke kikubwa tunapata cha halali....

Kuna time unapitia hata hamu za wanawake unakuwa huna kabisa kutokana na ugumu wa life hapa Dasalamu.

Mjini pazito 🙌 🙌 🙌 🙌
Mjini pazito kivipi?....fafanua aiseee.
 
Daaah mkuu ni kweli kabisa huku mjini bana ni vile tuna kaa kufata tittle ila hali halisi ndio hvo.

Japo mikoani napo daaah kutoboa kule ni hatari.

Hapa mjini uwezi kuta mtu ana teseka miaka na miaka.
Unapitia kipindi kidogo tu cha kukufunza baada ya hapo unaanza kula matunda ya dunia
Mjini si Dar tu! Acheni uongo uongo! Life is how you make it! Sio lazima kukomaa na Dar wakati unaweza kwenda Mwanza na ukakomaa na kutoboa!
 
Hiyo siyo" typing error", "typo" zinafahamika na ujinga unafahamika.

Mtu anaeshindwa kutofautisha hata R na L ni lazima mjini apaone "pazito".

Yote ipo kichwani kwa mtu.

Fikiria sisi tuliozaliwa na kukulia mjini utwambie mjini "pazito", tutakuelewa kweli?

Uzit na wepesi wa maisha upo mawazoni mwetu, siyo uhalisia.

"pazito" pana kilo ngapi na huko kwepesi pana kilo ngapi?
Yani R na L ndio sababu Tanzania bana Ila tutafika tu.
 
Mimi niko hapa Dar kitambo ndo maana Mo Dewji alisema vijana wa Dar wanazidiwa kipato na vijana wa mikoani!
Njombe,Kahama ,Mwanza kuna fursa nyingi endeleeni kuamini ujinga wa Mjini wakati hata huko ni mjini tu kwa maana ya huduma zote unapata!
Mbona yeye aendi kuwekeza njombe huko kaweka viwanda vyake dar hapa mkuu
Za kuambiwa changanya na zako
 
Mbona yeye aendi kuwekeza njombe huko kaweka viwanda vyake dar hapa mkuu
Za kuambiwa changanya na zako
Kaka acha uongo Tanzania maisha sio Dar tu!
Wengi wa vijana ni malimbukeni sana na wengi hawana ndoto wanaishi maisha ya kusadikika!
Dar ni mkoa kama mikoa mingine utofauti wa Dar ni jinsi gani unafanya kazi zako!
Nikukumbushe sehemu kubwa ya shughuli za Dar zinakonection na mikoani kwa hiyo Dar is nothing bila mikoa mingine!
Juzi kati tu hapa Kahama imeongoza Tanzania kwa makusanya ya kikodi unasemaje Dar ni bora kuliko Kahama wakati hata Dar unayokaa ni Mbagala au Kigogo!
 
Back
Top Bottom