Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Hali ya mjini hapa Dar es Salaam ni tofauti na nilivyofikiria

Huko ndio pazito mno kuliko hata dar maana fursa hakuna bahati mimi nilikuja tu na kampuni flani bila hivo nisingekaa huku ningekomaa na dar hiyo hiyo mpaka kieleweke
Mi mkuu ndo nakomaa unajua hizi ni hatua tuu mi sizani mpka mwakani hali itakua hivi hivi l.
Najua takuwa mahali fulani.
Hakuna kitu kinadumu milele.

Kwa magumu niliyopitia huko nyuma kwa sasa naona hii ni kawaida tu ila nachoogopa naona kama sitotoka kwenye ile poverty chain mkuu
 
Mungu azidi kutupigania na kweli ya kesho atuyajui cha msingi ni kuendelea kupambana tu nakumbuka mwaka jana miezi kama hii nipo tu maskani sina kazi pia sina geto wala chochote naamka asubuh naenda tu kushinda kariakoo na wana, lakini leo hii tayari kuna hatua nimepiga Mungu ni mwema tuendelee kupambana na kumwamini yeye
 
Bi mkubwa sina la kukuambia ila jua tu kuna watu hapa mjini wanahali mbaya kifupi mjini ni pazito mno..

Sasa wewe unapofocus na mambo ya typing error hi ni hali ya kushiba mkuu
Hiyo siyo" typing error", "typo" zinafahamika na ujinga unafahamika.

Mtu anaeshindwa kutofautisha hata R na L ni lazima mjini apaone "pazito".

Yote ipo kichwani kwa mtu.

Fikiria sisi tuliozaliwa na kukulia mjini utwambie mjini "pazito", tutakuelewa kweli?

Uzit na wepesi wa maisha upo mawazoni mwetu, siyo uhalisia.

"pazito" pana kilo ngapi na huko kwepesi pana kilo ngapi?
 
Sema mkuu maisha haya haya bana.
Tunaishi mara moja ngoja tupambane tuu.
Zamani nilikua naona watu wa dar wana roho mbaya sana ila sasa kwa hali hii najiona na mimi naenda kuwa hivo
Usiwe na roho mbaya ishi kwa code, fanya kile moyo wako unataka.

Roho mbaya si za watu wote mkuu, kama sio mambo zako usiige wala usiwe na roho mbaya kwa kupretent.
Waache wenye nazo wapete nazo.
 
Mungu azidi kutupigania na kweli ya kesho atuyajui cha msingi ni kuendelea kupambana tu nakumbuka mwaka jana miezi kama hii nipo tu maskani sina kazi pia sina geto wala chochote naamka asubuh naenda tu kushinda kariakoo na wana, lakini leo hii tayari kuna hatua nimepiga Mungu ni mwema tuendelee kupambana na kumwamini yeye
Daaha mkuu tunapambana hivo hivi Mungu yupo pamoja na sisi vijana.
Ila hali niliyoiona hata kule kariakoo.
Mkuu pesa zipo na kwenye watu ndo pesa zinapatikana ila sasa zinapatikana vipi hapo ndo code zilipo
 
Hiyo siyo" typing error", "typo" zinafahamika na ujinga unafahamika.

Mtu anaeshindwa kutofautisha hata na R na L ni lazima mjini apaone "pazito".

Yote ipo kichwani kwa mtu.

Fikiria sisi tuliozaliwa na kukulia mjini utwambie mjini "pazito", tutakuelewa kweli?

Uzit na wepesi wa maisha upo mawazoni mwetu, siyo uhalisia.

"pazito" pana kilo ngapi na huko kwepesi pana kilo ngapi?
Sasa kama umekulia mjini uwezi kusoma uzi wote huo we ukafocus kwenye tofauti ya R na L mkuu..
Ndo mana nimesema itakua umeshiba maza au tu ni vile unataka ligi..
Naelezea hali ilivyo hapa mjini wee kama unaona kwako mambo poa we pita hivi
 
Back
Top Bottom