Halikua lengo la Mungu binadamu tujisitiri tupu zetu. Pongezi kwa shetani

Halikua lengo la Mungu binadamu tujisitiri tupu zetu. Pongezi kwa shetani

Nguo ni matokeo ya dhambi. Mungu alikuwa ametuumba kwa utukufu bila kijifunika mavitambaa na timgekuwa timapendeza kama ndege, wanyama bao wote wapo uchi lakini hawsoni aibu Wala hatuwaonei aibu. Hivyo usije ukajinadibu na matambara unayojigunika gubigubi kuwa Mungu anapendezwa nayo
 
isome kwanza concept ya energy then ukiilewa njoo tuendelee na mjadala.
Hakuna sehemu yeyote kwenye Energy inayothibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Mnafosi fosi mawazo yenu na imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.

Na wewe ukiweza kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu ndio uje tuendelee na mjadala.
 
Ingekuwa tushazoea uchi tayari.

Kimbembe itokee sasa hivi Mungu asemehe kosa la Adam na tuanze tena kuwa uchi.

Kuna baadhi ya viumbe hasa vya kike havitotokà nje. Kuna miili mizuri ikifunikwa tu, ikiwa wazi kuna milima na mabonde, visiki na vihunzi. Huangalii mara mbili.

Na wale wahanga wa vibamia itakuwa fedheha nyingine. Unakutana na njemba mbavu halafu ana kinukta tu.

Kuna wale wakazi wa mbagala na gongolamboto, daladala zinavyokuwa nyomi, halafu upo nyama kwa nyama na mshangazi, ingekuwa ni mwendo wa kuchafuana tu.
 
Hakuna sehemu yeyote kwenye Energy inayothibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Mnafosi fosi mawazo yenu na imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.

Na wewe ukiweza kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu ndio uje tuendelee na mjadala.
Concept ya energy inathibitisha uwepo wa Mungu, ndo maana nikakueleza uisome ili tuwe na mjadala mzuri.
 
Sisi binadamu tungekuwa tuishi utupu tungekuwa wabaya sana na hii mitaimbo yetu... Ila tuseme ukweli biblia na quran hapo tulipigwa changa la macho
 
Wakuu,
Kutokana na maandiko(Quran na Biblia)
Turejee kilichotokea pale Eden Kwa binadamu WA kwanza ADAM na HAWA.

Baada ya ushawishi wa SHETANI, Adam na HAWA wanaamua kula tunda la mti wa kati waliokatazwa na Mwenyezi Mungu.

Na baada ya hapo, wanastuka kujikuta uchi na kutafta namna ya haraka ya kuzisitiri tupu zao.

Hii inatupa tafsiri kwamba halikua lengo la Mungu sisi binadamu tuzisitiri tupu zetu, Tulitakiwa kuishi uchi daima Kama viumbe wengine.

Tukumbuke pia, sio ng'ombe, sio mbuzi, sio kondoo Wala kiumbe yyt mwingine Duniani aliekula tunda lile pale Eden isipokua binadamu pekee Ambae ndie Hadi sasa anaezisitiri tupu zake.

Najaribu kuwaza, Ni aibu Sana. Binadamu mwenye akili zako timamu kumkemea na kumlaani SHETANI na KILA kinachomhusu shetani uku ukijisahau kwamba Hata hizo nguo zako ulizovaa kujisitiri hizo tupu zako Ni Kwa hisani yake yeye SHETANI.

My take:
Binadamu tuache na ule unafiki wa
"BANIANI MBAYA,KIATU CHAKE DAWA"

Namaanisha,
Kama kweli binadamu tumedhamilia kumkataa shetani na Kila kitu CHAKE. Basi tuanze rasmi kuishi na kutembea uchi (Nudism) Kama viumbe wengine duniani maana Tangu mwanzo halikua lengo la Mwenyezi Mungu sisi binadamu tuzisitiri nyeti zetu.

Nawasilisha tujadili Kwa hoja🙏
Kwahiyo hilo tunda lilikua ni tunda gani kwanza ambalo liliwafanya hao watu wakuitwa binadamu wa kwanza waanze kuvaa nguo?

Anyway ila mimi nadhani asili ya uumbaji wa mwanadamu ni kuhakikisha anaumbwa kwa mfano wa waliomuumba ila nguvu za kiungu zinawekwa codes ili kumfanya aweze kuwa mtiifu na kufuata orders kutoka kwa waliomuumba.

Kiasili mwanadamu ako na pande kuu mbili upande wa roho na huu wa damu na nyama.

Upande wa damu na nyama ni upande ambao unamuunganisha mwanadamu na dunia Kwahiyo mambo yote ambayo huwa tunajifunza kwa kuona, kusikia na hata kusoma na kuyaweka kichwani huwa yanatufanya tuzamie kwenye huu ulimwengu ambao sisi wote ni wageni na kusahau asili yetu na dhumuni mama la uwepo wetu hapa.

Na Upande wa roho ndio upande wenye nguvu kwa mwanadamu na huu ndio upande ambao kama mtu utaamua kujiungamanisha nao moja kwa moja basi utakua na uwezo wa kufungua codes nyingi mficho ambazo wote tumeumbwa nazo na kuwasiliana moja kwa moja na malaika walio kwenye njia za mitetemo yako ya kiroho.

Sasa ukirudi pale bustanini tunaambiwa kwamba kabla hawajala tunda walikua na uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na aliyewaumba it means nyakati hizi nguvu zao za kiroho zilikua kubwa kuliko za kilimwengu kwani tunaona baada ya kula tunda wakapoteza uwezo wakuskia ile sauti ya aliyewaumba.

Hapa inamaanisha kwamba shetani aliamua kumbadilisha binadamu kutoka kuishi zaidi kwenye ulimwengu wenye nguvu ambao ndio unamuunganisha na asili yake na kumleta kwenye ulimwengu mpya ambao ameletwa kwaajiri ya lengo maalumu.

Sasa inawezekana ni kweli shetani alikupa codes zilizohamisha uwezo wako wa nguvu kutoka kwenye mitetemo ya juu sana hadi kuja kwenye mitetemo hafifu na kuanza kufanya mambo yako kwa kujiamulia mwenyewe na si kufuata orders kama ilivyokua mwanzo.

Ila sasa faida ya hii ni uhuru wa kufanya mambo yako kwa kujiamulia mwenyewe ila unakua uko kwenye pumbaziko kubwa ambalo linafanya watu waliowengi hapa duniani wasijue hatima za wao kuwa hapa ni zipi.

Wengi wanadhani tupo hapa kwaajiri ya kuvaa kama wewe uwazavyo ndugu mwandishi au kula kunywa na kutafuta pesa kisha tuzaliane na baadae turudi tulipotoka ila kiuhalisia sio kweli bali kila roho iliyopo kwenye mwili wenye umbo la kibinadamu ipo hapa kwaajiri ya kutimiza lengo maalumu ambalo hilo ndilo hatima yake.

Kwa maana hiyo basi nguo ni kitu kidogo sana ambacho hakifikii hata size ya punje ya haladani ya power ambayo ilipotea kufuatia tukio lile la pale bustanini.

NB:
Haya ni mawazo ambayo nimeyaleta kwa sauti ila yamejengwa juu ya maandiko ya hilo tukio lenyewe na tafakari yake ikanifikisha kwenye engo hii.
 
Concept ya energy inathibitisha uwepo wa Mungu, ndo maana nikakueleza uisome ili tuwe na mjadala mzuri.
Inathibitishaje uwepo wa huyo Mungu?

Hakuna uhusiano wowote ule wa Energy na Mungu.

Unachofanya wewe ni Logical non sequitur.

Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.
 
Mwanzo 3:22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya;

1. Akawa mjuaji
-akili ziliongezeka,
(Binadamu alitoroka kutoka kwenye umbumbumbu)
-yaani ilibaki sekunde mwanadamu atoroke kifo.
 
Nguo ni matokeo ya dhambi. Mungu alikuwa ametuumba kwa utukufu bila kijifunika mavitambaa na timgekuwa timapendeza kama ndege, wanyama bao wote wapo uchi lakini hawsoni aibu Wala hatuwaonei aibu. Hivyo usije ukajinadibu na matambara unayojigunika gubigubi kuwa Mungu anapendezwa nayo
Ushaliona kende la nyani linavotisha?
 
Back
Top Bottom