Uchaguzi 2020 Halima Mdee, fedha za mfuko wa jimbo umepeleka wapi?

Hahaha mwambie Lisu amuulize Lowasa mpaka sasa lisu hajakuta hata nusu ya nyomi ya Lowasa lakin alishindwa sembuse lisu yule Uraisi ataendelea kuota tu ndotoni ila hawezi kuwa rais Kamwe Magufuli oyeeeeee
 
Aliyemshauri Halima kuandika kile kitabu amemponza sana aise Anguko la Halima tar 28
 
Kiukweli sasa imetosha halima kutuibia bora tuende na gwajima safari hii
 
Tarehe 28.10.2020, wananchi wa Tanzania watakuwa katika moja ya majukumu makubwa ambayo pia ni haki na wajibu wao kumchagua kiongozi wanayemtaka ambaye atawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano mingine. Wakati kampeni zikiwa zinaendelea za urais, wabunge na madiwani; nikusogezee hali inavyoendelea katika jimbo la Kawe.

Jimbo limekuwa chini ya CHADEMA kwa miaka 10 likiongozwa na mbunge mwanamke Halima James Mdee. Kwa miaka 10 mambo yamekuwa mazuri kwake na huenda alijisahau kwamba maisha yanavyosonga mbele, uelewa unaongezeka, watu wanaendelea kupambanua akili zao na hivyo ni rahisi sana kugundua kuwa wamekuwa wakiibiwa kwa kipindi chote hicho.

Hii inaweka alama nyingine ambayo inaashiria kuwa huenda safari ya kisiasa kwa Halima Mdee ndani ya jimbo la Kawe imefikia mwisho na wananchi wako tayari kubadilisha hali zao kwa kumchagua mtu mwingine anayeonekana kuwa na ushawishi mkubwa na uwezekano wa kutatua matatizo yao.

Jambo linaloshangaza sana ni wanachama wa CHADEMA kuwa mstari wa mbele kuwashawishi wananchi wasimchague Halima kwa kile wanachokisema kuwa wao husahaulika baada tu ya uchaguzi. Hapa awali limeonekana wimbi kubwa la wanachama wa CHADEMA wakitimkia CCM na wote wana kauli moja,"HALIMA UMESAHAU NINI KAWE?, NI ZAMU YA GWAJIMA SASA.

Joseph Sospeter
Kawe-Ukwamani
 

Hii ni kengele kuwa mdee hafai kuchukua jimbo tena, kawe haiko tena mikononi mwake
 
Mzee kapiga magoti Jana huko iringa taarifa unayo?
Acha ushamba ile n Ishara ya unyenyekevu sasa mnajidanyanga kuwa Lisu atashinda pole yenu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]hamtaamin tar 28 ila hamchelewi kusema uliibiwa kura maana ndo zenu
 
Hahah kwakweli ameshakufa kisiasa na hawezi kufufuka tena mdee
Hatumtaki kabisaaaa
 
Niliongea na Halima mara nyingi kuhusu hili, ila shida ambayo anayo ni mtu wa kupuuza sana.
Bado nina imani anaweza kushinda, ila asipuuze anachoambiwa maana huwezi jua ukweli upo kiasi gani
 
Kama kuna sehemu ambayo itakuwa changamoto kwa sasa ni kuendelea kumsapoti huyu Halima wakati tunafahamu kuwa hana alichofanya jimboni. Mimi kama kada wa CHADEMA halima simtaki bora kura yangu nimpe GWAJIMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…