Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wambie tu Halima.Mbunge wa viti maalum Halima Mdee amesema kama kauli za kisiasa zinazotolewa na viongozi zikifuatiliwa basi yawezekana viongozi wote wakawa wahaini.
Mdee amesema kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha BBC na kueleza kuwa yeye hajajua kama kilichofanya kukamatwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ni kauli alizotoa au kuna jambo lingine.
"Kama kuna mengine yamejificha mimi sijui lakini kama ni hizi kauli za kisiasa tukianza kurejea kauli za kisiasa za kila kiongozi wa CCM wa CHADEMA na hivi vyama ambavyo viko active tutakua wahaini wote kama ni kauli hizo"
Halima anajua kabisa kuna jambo lingine. Nadhani wamesikia.Mdee amesema kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha BBC na kueleza kuwa yeye hajajua kama kilichofanya kukamatwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ni kauli alizotoa au kuna jambo lingine.
kwani halima hujui kuwa lengo ni kuzima nguvu ya Lisu? Sio kuwa hawajui, wanajua fika na nina uhakika hata mahakama Lisu atashinda!Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, amehoji mantiki ya kesi ya uhaini inayomkabili mwanasiasa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akisema kauli za kisiasa haziwezi kufasiriwa kama uhaini bila ushahidi wa ziada.
Akizungumza kuhusu kesi hiyo, Mdee alisema “Katika mazingira ya kawaida, kauli za kisiasa zinajulikana ziko wazi na uhaini ni jambo zito kama ulivyosema. Tukianza tukirejea kauli za kisiasa za kila kiongozi kuanzia wa CCM, wa CHADEMA na vyama vingine, basi tutakuwa wahaini wote.”
Mdee amesema hana taarifa iwapo kuna ushahidi mwingine wa siri unaomhusisha Lissu zaidi ya kauli zake, lakini amesisitiza kuwa kama ni kauli tu, basi hoja ya uhaini haipaswi kusimama.
Chanzo: BBC Swahili
Rudia kusoma ulichoandikakwani halima hujui kuwa lengo ni kuzima nguvu ya Lisu? Sio kuwa hawajui, wanajua fika na nina uhakika hata mahakama Lisu atashinda!
Uasi si lazima iwe kupindua serikali, unaweza kuasi kutofuata sheria kandamizi, na hii siyo kuwa na nia ya kupindua serikali!
Ccm oyeeeMbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, amehoji mantiki ya kesi ya uhaini inayomkabili mwanasiasa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akisema kauli za kisiasa haziwezi kufasiriwa kama uhaini bila ushahidi wa ziada.
Akizungumza kuhusu kesi hiyo, Mdee alisema “Katika mazingira ya kawaida, kauli za kisiasa zinajulikana ziko wazi na uhaini ni jambo zito kama ulivyosema. Tukianza tukirejea kauli za kisiasa za kila kiongozi kuanzia wa CCM, wa CHADEMA na vyama vingine, basi tutakuwa wahaini wote.”
Mdee amesema hana taarifa iwapo kuna ushahidi mwingine wa siri unaomhusisha Lissu zaidi ya kauli zake, lakini amesisitiza kuwa kama ni kauli tu, basi hoja ya uhaini haipaswi kusimama.
Chanzo: BBC Swahili
Kuna kipi ambacho wewe hukuelewa hadi "arudie kusoma alichoandika". Siyo wewe unayetakiwa kurudia kusoma kilicho andikwa na kuelewa maana yake ni nini?Rudia kusoma ulichoandika
Kama umejifunga kajifungue!! Hayo maelekezo sio yakoKuna kipi ambacho wewe hukuelewa hadi "arudie kusoma alichoandika". Siyo wewe unayetakiwa kurudia kusoma kilicho andikwa na kuelewa maana yake ni nini?
Ndiyo, sheria kama ni "kandamizi" watu watazikataa. Kuna lipi la ajabu hapo!
Wananchi wakizikataa hizo sheria kandamizi kwa kuwaondoa viongozi waliozisimamia waitwe "waasi"?
Fr Kitima aliwaambia hivyo ccm, wao wakaona dawa ni kumshambulia.Huo ndo ukweli, wanajitoa ufahamu tu.
Kama uhaini ni kujinyakulia madaraka kinyume na taratibu, WiZI wa kura ni uhaini
Lakini amejibu maswali yote vizuri sana,,Halima huelewi neno KUBAMBIKA?