Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Vipi huyu,ni Malaya wa nini?View attachment 1638986
Kama wewe ni mwanaume na hauna picha hata moja ya ukiwa umekumbatiwa na mwanamke(rafiki, mke, binti yako, mfanya kazi mwenzako, mwanafunzi mwenzako, mwana kwaya mwenzako, bar maidi, mpango wa kando n.k.) basi una matatizo. Na hivyo hivyo kama wewe ni mwanamke. Acheni unafiki.

Amandla...
 
Wameomba radhi au ndio, wanasemaje kwenye huo mkutano wao?
 
Wana hara hara tu hawa mama zetu na wadogo zetu! Wamerubuniwa, wameingia mkenge. MZEE MDEE bila haya unatuambia tusome Zaburi: 35 wakati unakula wanawake wa BAVICHA!

Mmepewa ubunge kinyume na katiba, mmeapishwa gereji na aliyewaapisha kumpiga vijembe aliyekuwa mwenyekiti wako [Mbowe].

Mzee HALIMA tunakushauri uanzishe chama kipya na jina liwe COVID-19.
 
Imekuuma, Mbowe ni funding sana huko chini
 
Mpaka Hapa Kwa namna alivyoongea Mdee, naiona busara yake na anastahili kuwa MK Chama ama KM Chama, kawazidi wote waliopo kwenye nafasi hiyo.

Waliopo ni wakurupukaji na si waonyesha njia, Uongozi si mihemko, Uongozi ni Hekima na kiongozi hupimwa ktk kutatua Changamoto na si vinginevyo
 
MATAGA , Mnataka Mdee awe Mwenyekiti amuondoe Mbowe, aluu, hata Membe anafaa kuwa mwenyekiti wa CCM kwa busara zake na utulivu wake, hata namna anavyoongea kingereza.
 
Sasa tueleze ukweli ilikuwaje hadi ukatuingiza kwenye sintofahamu hii. Weweni kiongozi wa ngazi ya kitaifa. Unaelewa na uneshawahi kushiriki kwenye mchakato wa kuteua wabunge wa viti maalum. Imekuwaje leo ukaamua kukuteua na kwenda kuapishwa na Ndugai kwa utaratibu unaovunja katiba?
 
Halima unasema waliokuwa viongozi wako ni waongo! Kwa neno hilo hauwezi kupata suluhu, insubordination ya kwanza mlipokataa wito na hii ya kuwaita waongo inakazia uhalali wa kufukuzwa uanachama. Halima, fafanua jinsi utakavyoendelea uanachama wako chini ya viongozi wako waongo! Au mtafanya mapinduzi na nyie kuwa viongozi wa CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…