Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Kiukweli Hukumu ziko Kenya bhana tena mubashara kwa TV [emoji23][emoji23]

Na kule akina Mbowe na wenzake wakiendelea kuvuta ruzuku kila mwezi inayotokana na akina Mdee kuwepo bungeni. Na wakileta fyoko kukata rufaa, hiyo kesi itamalizika 2027, wallahi tena.
 
Mbowe alifikiri chama ni cha mkwewe, akaona anaweza kuwaburuza watu apendavyo.
 

Wavunja katiba hata ya chama chao hawa ndiyo maana mwaka umeisha fyuu hakuna uchaguzi mkuu, Mbowe anaendelea kutamba!
 

..uhalali wa maamuzi ya Baraza kuu la Chadema unatokana na idadi ya wajumbe wake kuwa wengi kuliko idadi ya wajumbe wa kamati kuu ambao walitoa hukumu ya awali. Masuala ya vyama huamuliwa kwa KURA za wajumbe na uhalali wake inatokana na mazingira hayo.
 
Huyo Mbowe hamna kitu hapo boss. Ni muda sana Mbowe ameshaflop. Na kwa taarifa yako uwepo wa hao COVID huko bungeni una mkono wa Mbowe kwa namna moja au nyingine.
Si kweli
 
Hayo ya kwako chombo cha kutoa haki kimeshatoa haki kama hukupendezwa si ukate rufaa
Kwani kesi zinaendeshwa ili kubalance, kwamba leo ukishinda, ni halali kesho kushindwa? Sikutegemea hukumu tofauti na hukumu hiyo ya mahakama kibogoyo.
 
Ruzuku za vyama vya siasa hazitokani na wabunge wa viti maalum
Kwa akili yako unaamini kabisa yule mbunge mmoja wa jimbo la NKANSI ndiye anasababisha Msajili wa vyama awape hayo Mabilioni mnayopata!! Check your arithmetic bro
 
Nilijua tu itakua hivi.

Yule mwendawazimu alivuruga uchaguzi kwa ushamba wake akajisombea majimbo yote huku akiwa ana mpango wa kujiongezea muda.

Kuja kushtuliwa kuwa nchi itakosa baadhi ya mikopo ndio akaangukia kwa hao Covid 19 walioapishwa kwenye parking ya gari.
 
Kwamba wajumbe wa kamati kuu waliotoa hukumu, hawapaswi kuwa sehemu ya baraza kuu linalosikiliza rufaa ya kamati kuu. PRINCIPLE OF BIASNESS.

Very logical reasoning.
Majinga ya cdm yanapinga eti
 
Nilijua tu itakua hivi.

Yule mwendawazimu alivuruga uchaguzi kwa ushamba wake akajisombea majimbo yote huku akiwa ana mpango wa kujiongezea muda.

Kuja kushtuliwa kuwa nchi itakosa baadhi ya mikopo ndio akaangukia kwa hao Covid 19 walioapishwa kwenye parking ya gari.
 

Kwa hili suala inapaswa ajiuzulu, inatosha sasa. Cha ajabu baraza kuu halitoitwa mpaka mwakani June kuja kujadili hukumu ya leo? Aisee huyu jamaa atupishe.
Kwani hii ilikuwa Mahakama ya Rufaa yenye uamuzi wa mwisho katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mbona hukumu nyingi tu hutenguliwa rufaa ikikatwa? Sema tu kama kusema tu kama hao 19 walifukuzwa ubunge kiuhallali au la imechukua nadhani mwaka mzima na zaidi ni shida zaidi. Kesi ya kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta ilikuja nyuma na ile kesi iliamriwa ndani ya wiki moja. Hii ya akina Halima sijui kwa nini ilichukua muda mrefu hivyo.
 
Kwa hili suala inapaswa ajiuzulu, inatosha sasa. Cha ajabu baraza kuu halitoitwa mpaka mwakani June kuja kujadili hukumu ya leo? Aisee huyu jamaa atupishe.
Kabisa. Huyu ni muda tu alishachoka. Mimi baada ya blunder ya Lowassa nilijua hakuna mwenyekiti sahihi hapo. Anyway tumevumilia Hadi uchaguzi mkuu wa chama uliopita hakustahili tena. Kwa sasa anaendelea kwa sababu anazojua yeye, lakini sio kukiimarisha chama. Alisema hii 2023 ataachia uenyekiti, lakini naona kajikausha akidhani tumesahau.
 
Ni aina ingine ya mambo ya hovyo hovyo kwa kigezo kua haki ionekane imetendeka.

Mambo kama haya ndio hufanya watu wa ngozi nyeupe watuone kama hatujitambui, tunahangaika na mikopo ya wafadhili, fedha inaenda kutumbuliwa na wasanii kama hawa.

Iko clear kua ni kutafuta justification ya kuwa tuna bunge la vyama vingi. May be mwenye akili aniambie hawa watu wanamuwakilisha nani bungeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…