Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Kiukweli Hukumu ziko Kenya bhana tena mubashara kwa TV [emoji23][emoji23]

Na kule akina Mbowe na wenzake wakiendelea kuvuta ruzuku kila mwezi inayotokana na akina Mdee kuwepo bungeni. Na wakileta fyoko kukata rufaa, hiyo kesi itamalizika 2027, wallahi tena.
 
Mbowe alifikiri chama ni cha mkwewe, akaona anaweza kuwaburuza watu apendavyo.
 
CHADEMA watakuwa wanvunja katiba ya Nchi, hicho kitu hakipo, katiba inalindwa kwa jasho na damu.
Ni upuuzi uliopitiliza kama utashindwa kwa vitu vidogo kulinda katiba, sasa akija Yule mama wa Malawi wewe si ungemuachia ziwa Nyasa alokuwa anataka kulichukua 2016, au Iddi amini wewe si ungemuachia Kagera kwa kigezo kuwa Tanganyika ni kubwa?

Wavunja katiba hata ya chama chao hawa ndiyo maana mwaka umeisha fyuu hakuna uchaguzi mkuu, Mbowe anaendelea kutamba!
 
Mahakama inayohaki ya kuzichallenge katiba zozote za taasis. Pili mtu asipohisi kutendewa haki na taasisi ni mahakama ndio yenye haki ya kupitia maamuzi-unadhani taasisi hizi zisingehojika, watu wake ukandamizwaji ungekuwaje? Nasema haya bila kukwepa ubovu wa mahakama zetu. Tatu hata hukumu hii imeangalia uhalali wa wajumbe wa baraza kuu ndio maana ikahitimisha ilikuwa ni impartial.

..uhalali wa maamuzi ya Baraza kuu la Chadema unatokana na idadi ya wajumbe wake kuwa wengi kuliko idadi ya wajumbe wa kamati kuu ambao walitoa hukumu ya awali. Masuala ya vyama huamuliwa kwa KURA za wajumbe na uhalali wake inatokana na mazingira hayo.
 
Huyo Mbowe hamna kitu hapo boss. Ni muda sana Mbowe ameshaflop. Na kwa taarifa yako uwepo wa hao COVID huko bungeni una mkono wa Mbowe kwa namna moja au nyingine.
Si kweli
 
Hayo ya kwako chombo cha kutoa haki kimeshatoa haki kama hukupendezwa si ukate rufaa
Kwani kesi zinaendeshwa ili kubalance, kwamba leo ukishinda, ni halali kesho kushindwa? Sikutegemea hukumu tofauti na hukumu hiyo ya mahakama kibogoyo.
 
Ruzuku za vyama vya siasa hazitokani na wabunge wa viti maalum
Kwa akili yako unaamini kabisa yule mbunge mmoja wa jimbo la NKANSI ndiye anasababisha Msajili wa vyama awape hayo Mabilioni mnayopata!! Check your arithmetic bro
 
Nilijua tu itakua hivi.

Yule mwendawazimu alivuruga uchaguzi kwa ushamba wake akajisombea majimbo yote huku akiwa ana mpango wa kujiongezea muda.

Kuja kushtuliwa kuwa nchi itakosa baadhi ya mikopo ndio akaangukia kwa hao Covid 19 walioapishwa kwenye parking ya gari.
 
Nilijua tu itakua hivi.

Yule mwendawazimu alivuruga uchaguzi kwa ushamba wake akajisombea majimbo yote huku akiwa ana mpango wa kujiongezea muda.

Kuja kushtuliwa kuwa nchi itakosa baadhi ya mikopo ndio akaangukia kwa hao Covid 19 walioapishwa kwenye parking ya gari.
 
Haya hapa ni baadhi ya Maelezo ya Jaji .

View attachment 2842497
Kama tulivyotarajia , Jaji ameamua hivi .

View attachment 2842542

====

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imewapa ushindi Halima Mdee na wenzake 18 kwenye kesi yao waliyoiwasilisha Mahakamani hapo dhidi ya Uamuzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa kuwafukuza uanachama Wabunge 19 wakituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chama.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea

Kwa hili suala inapaswa ajiuzulu, inatosha sasa. Cha ajabu baraza kuu halitoitwa mpaka mwakani June kuja kujadili hukumu ya leo? Aisee huyu jamaa atupishe.
Kwani hii ilikuwa Mahakama ya Rufaa yenye uamuzi wa mwisho katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mbona hukumu nyingi tu hutenguliwa rufaa ikikatwa? Sema tu kama kusema tu kama hao 19 walifukuzwa ubunge kiuhallali au la imechukua nadhani mwaka mzima na zaidi ni shida zaidi. Kesi ya kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta ilikuja nyuma na ile kesi iliamriwa ndani ya wiki moja. Hii ya akina Halima sijui kwa nini ilichukua muda mrefu hivyo.
 
Kwa hili suala inapaswa ajiuzulu, inatosha sasa. Cha ajabu baraza kuu halitoitwa mpaka mwakani June kuja kujadili hukumu ya leo? Aisee huyu jamaa atupishe.
Kabisa. Huyu ni muda tu alishachoka. Mimi baada ya blunder ya Lowassa nilijua hakuna mwenyekiti sahihi hapo. Anyway tumevumilia Hadi uchaguzi mkuu wa chama uliopita hakustahili tena. Kwa sasa anaendelea kwa sababu anazojua yeye, lakini sio kukiimarisha chama. Alisema hii 2023 ataachia uenyekiti, lakini naona kajikausha akidhani tumesahau.
 
Ni aina ingine ya mambo ya hovyo hovyo kwa kigezo kua haki ionekane imetendeka.

Mambo kama haya ndio hufanya watu wa ngozi nyeupe watuone kama hatujitambui, tunahangaika na mikopo ya wafadhili, fedha inaenda kutumbuliwa na wasanii kama hawa.

Iko clear kua ni kutafuta justification ya kuwa tuna bunge la vyama vingi. May be mwenye akili aniambie hawa watu wanamuwakilisha nani bungeni?
 
Back
Top Bottom