Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao

Mahakama haijawa realistic kwenye uhalisia wa mambo. Kwa Tanzania huwezi kuwa mjumbe wa kamati kuu na usiwe mjumbe wa Baraza kuu bila au mjumbe wa halmashauri kuu. Sasa unataka mwenyekiti, Katibu mkuu, makamu mwenyekiti nk wasishiriki Baraza kuu wakati wao ni wajumbe Kikatiba? Mahamaka imewalinda akina mdee.
Lakini kisheria huwezi kuwa mtoa hukumu ya kwanza halafu pia ukawepo wakati wa kusikiliza rufaa.
 
Mahakama haijawa realistic kwenye uhalisia wa mambo. Kwa Tanzania huwezi kuwa mjumbe wa kamati kuu na usiwe mjumbe wa Baraza kuu bila au mjumbe wa halmashauri kuu. Sasa unataka mwenyekiti, Katibu mkuu, makamu mwenyekiti nk wasishiriki Baraza kuu wakati wao ni wajumbe Kikatiba? Mahamaka imewalinda akina mdee.
Law is about Principles. Na ndio mahakama imesimamia. Sasa ulitaka mahakama ihalalishe uvunjaji wa kanuni za haki asili kwa sababu tu setup ya vikao vya chama havitenganishi wajumbe?

Message ya hukumu hii ni kuwa miundo ya halmashauri/mabaraza makuu ya vyama hayafai kuwa vyombo vya rufaa vya kamati kuu. It's a precedent ambayo msajili[angekuwa na weled] alipaswa arekebishe kwenye vyama.
 
Chadema bhana 😂 itafika 2050 na bado mtaendelea kumlaumu JPM, michongo yote ifanywe na mume wenu Mbowe halafu mnakuja kumlalamikia JPM
NA BADO MTALALAMIKA SANA TUUU.

Yule ndio chanzo tuongee ukweli bila unafiki. Uchaguzi ungeenda fair mengine haya kijinga yasingetokea.
 
Law is about Principles. Na ndio mahakama imesimamia. Sasa ulitaka mahakama ihalalishe uvunjaji wa kanuni za haki asili kwa sababu tu setup ya vikao vya chama havitenganishi wajumbe?

Message ya hukumu hii ni kuwa miundo ya halmashauri/mabaraza makuu ya vyama hayafai kuwa vyombo vya rufaa vya kamati kuu. It's a precedent ambayo msajili[angekuwa na weled] alipaswa arekebishe kwenye vyama.

Hapo nakuelewa. Ila unafanyaje kwa Sasa kutenda haki kwa chama? Mahakama ingejikita kwenye haki na sio Principles ambazo ni more theoretical.
 
Haya hapa ni baadhi ya Maelezo ya Jaji .

View attachment 2842497
Kama tulivyotarajia , Jaji ameamua hivi .

View attachment 2842542

====

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam imewapa ushindi Halima Mdee na wenzake 18 kwenye kesi yao waliyoiwasilisha Mahakamani hapo dhidi ya Uamuzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa kuwafukuza uanachama Wabunge 19 wakituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chama.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati Kuu iliyowafukuza kuwa tena wajumbe wa Baraza kuu ambalo lilisikiliza rufaa yao kinaondoa uhalali wa maamuzi ya Baraza Kuu "Baraza Kuu lilikwenda kinyume na kanuni ya kawaida ya kutokupendelea
Tuliyategemea hayo majibu kwa hisani ya spika na ccm kulinda legacy ya mwendaxake
 
Kuna wakati najiuliza huu uvunjwaji wa katiba na taratibu za chama uliosemwa na jaji ulifanywa na chama chenye magwiji ya sheria kama inavyosemwa??? Hivi profesa Safari na Lissu walikuwa sehemu ya haya??? Kama jibu ndiyo, itoshe kusema hapana kwa wanachodai wanapigania
 
Chadema wakitoa hukumu upya kwa kufuata ushauri wa Mahakama hiyo maana yake ni kati ya March 2024, Akina Halima wataenda Mahakamani kupinga hukumu hii na kesi hii huenda isichukue muda mrefu kama hii wa miaka mitatu ila huenda ikachukua walau miezi 18.

na kwa kawaida Kiinua mgongo huwa kinalipwa mapema mapema mwa 2025.

Halima na Freeman hawajakutana Ufipa Street.

Halima James Mdee atakuwa Mbunge kwa Miaka 20 mfululizo. si haba

kuna Mtoto anazaliwa hadi anafika chuo kikuu bado anasoma jina la Mdee linaanza na Neno Mbunge

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Hapo nakuelewa. Ila unafanyaje kwa Sasa kutenda haki kwa chama? Mahakama ingejikita kwenye haki na sio Principles ambazo ni more theoretical.
Kaka wewe unachosema sheria iwe ni busara na sio msumeno.

Sijui hukumu imeelekeza vipi. Ila ninachokiona baraza kuu la chadema inabidi liitishwe upya bila wajumbe wa kamati kuu. Ndio ngoma iamuliwe.

Hili jambo chadema wawe nalo makini. CCM wanaweza watengenezea sarakasi wakafika serikali za mitaa wakiwa wamevurugana.
 
Ni Spika wa chama Cha wabunge kimataifa sio duniani. Bunge ni sovereign huwezi kuwa Rais wa mabunge duniani. Uwe muelewa.
Mbona Chama cha Demokrasia kiliwahi kuteua Mgombea urais 2015 bila ya kufuata Demokrasia inachojinasibisha nacho ?

walikutana DJ na Mzee wa Ufufuo wakayapanga na wengine wote wakaitwa kujulishwa ndio Mgombea akaambiwa haya njoo ujiunge na bado wakaendelea kutumia neno Chama cha Demokrasia

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom