Ndugu
Chagu wa Malunde hakuna chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria Tanzania kinachoitwa CDM...
Na bila shaka hapa ulikuwa unamaanisha
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo abbreviated as
CHADEMA, au siyo..?
Hili kosa la kiuandishi linafanywa mara kwa mara na watu wengi sana.
Contextually humu mtu akiandika
CDM akimaanisha
CHADEMA, likely anaweza kueleweka na wasomaji wenzake..
Lakini inakuwa ni makosa makubwa kuandika CDM katika nyaraka rasmi...
Na hili kosa ndilo lililotumiwa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali la mitaa wa mwaka 2019 kuwaengua baadhi ya wagombea wa CHADEMA kwa kuandika CDM ktk fomu zao za kuombea uteuzi mahali walipopaswa kuandika CHADEMA kama chama kinachowadhamini kugombea nafasi zao...
Si ajabu wengine wapo humu humu JF and they're still making the same horrible mistake...
CDM siyo CHADEMA na CHADEMA sio CDM. Hivi ni vyama viwili tofauti kabisa. Kimoja kimesajiliwa kisheria huku kingine hakijulikani ni nini na ni cha wapi..
Kwa uzi huu, mimi nimejikita hapa tu.
Hata hivyo kuhusu maamuzi ya Jaji, literally hukumu yake ilipaswa itamke hivyo.
Kinachofanyika ni kuwa, hata mahakama zetu zilishaingiliwa na ugonjwa wa siasa. Jaji badala atamke hukumu moja kwa moja kama inavyopaswa kutamka kwa sababu ndivyo ilivyo, yeye anacheza na maneno kwa kuusema ukweli kwa kuuficha bila ulazima wowote wa kufanya hivyo..