Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Tusibishane sana hapa, utaratibu wa kawaida unajulikana ofisi zote hufanya kazi kwa barua, hii ni kwa ajili ya records mbele yabsafari zikihitajika, na sio vinginevyo.

Suala la Happi na polisi huo ni ujinga tu wa CCM na mawakala wao, usiubebe huo ukaupeleka kwenye mambo mengine ya kawaida, utafeli.
Ndio nakuelewesha kwamba hicho ni kivuli tu mbona barua ya kuwatimua kina Lwakatare ilikataliwa kwamba minutes haziko properly arranged!!!

Na hiyo barua tutaambiwa font haisomeki, karatasi sio A4 etc. Lakini kwa CCM hayo ya compliance huwa hayafuatiliwi kabisa unakuta Lissu akikosoa serikali mtandaoni anakamatwa ila akisema mtandaoni anataka kuuawa anaambiwa "Polisi Hatufanyii kazi taarifa za mtandaoni".

Tuache double standards, Sheria zifuatwe kwa pande zote sio kwa upinzani ndio wanakua critical ila kwa CCM na Lipumba hukumu ilitekelezwa ndani ya lisaa limoja ya press release.
 
Hawa watu hawana aibu kabisa, mfumo unakutema wewe unalazimisha tu, hii ni mbaya sana kama binadamu mwenye akili timamu.
 
Kukiri kuipokea ni dispatch book na si vinginevyo au kugongewa muhuri wa received na signature kwenye copy of original.
Pamoja na hayo lazima akiri bungeni kuwa amepokea. Na atalifanyia maamuzi.
Apewe muda!
 
Kodi zetu na MATOZO mkuu , haina shida vipi?! Wanalipwa pesa haramu sio poa hata kidogo na haivumiliki.
Hakuna kodi au Tozo ambazo zimetumika sawia mpaka sasa, hizo tozo ni mbinu za kutafuta nauli za mama yenu anazotumia kufanya tour mwaka mzima.
 
Kweli katiba mpya pekee haitoshi!!
Sheria zipo hazifuatwi...tuanze kufundishana kuwalazimisha watawala kufuata sheria.

Sasa Bi Mkora anajipendekeza kuongea na Mbowe ili iweje wakati anaendekeza upumbavu kama huu?!
Bob mazishi ndiyo analazimisha kuongea na Samia.
 
mshawafukuza basi inatosha msiendelee kuwafatafata.wanasiasa wa kweli ni wachache sana waliowengi ni njaa tu.
wajinga ni wale waliopata majera,kufa au kufungwa jela kwaajili ya kupigania siasa za njaa kama za hawa wapinzani wa tz.
na waliowafunga, kuwaua na kuwateka ni ccm na genge lake
 
Ruzuku ya chama inalipwa kulingana na wastani wa kura chama kulipata kwenye uchaguzi wa 2020, sio uwepo wa wabunge wako ndani ya bunge.

Lakini yote kwa yote, CHADEMA ilishakataa kupokea ruzuku yoyote inayotokana na matokeo ya uchaguzi wa 2020. Na mpaka leo hii haijawahi kupokea ruzuku yoyote.
Ok,sasa ikitokea hawa wabunge 19 wakafukuzwa bungeni,je CDM itapeleka wabunge wapya waliofuata taratibu za chama kuwa wabunge?
Isipopeleka tutajua ni msimamo mzuri wa chama,ikitokea wakapeleka,je itafanya huo uchaguzi uliopita kuwa halali?
 
Bado wapo jengoni. Hawajafukuzwa.
..baraza kuu la chadema limeshathibitisha kuwavua uanachama.

..uamuzi huo ulifanyika kwa uwazi, wahusika walikuwepo, na vyombo vya habari vilishuhudia.

..hawa kina mama wawe WAUNGWANA. Kuendelea kwenda bungeni ni kuvunja sheria na kufanya vurugu.

..Ni aibu kwa MAMLAKA zetu kuwaacha wahudhurie bunge.
 
Huu ni mwaka wa pili katiba inavunjwa na hakuna kilichotokea.
Kuna msemo unasema ukitenda sawa sawa na kwa haki unaitendea NAFSI yako.
Na vilevile ukitenda uovu hujamtendea mwingine ni umeitendea nafsi yako.

Muda waja yatakuja kutokea makubwa kwa upande wao na hawata kuwa na la kufanya wala hakuna kitakachotokea vilevile.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Samia awe makini sana hasa wakati huu anaposisitiza maridhiano, kitendo cha kuendelea kuwaweka bungeni hao wanawake itatafsiriwa ni dharau, muhimu awe na heshima kwa mwenzake kama naye anavyotaka kuheshimiwa.
 
Mnachezewa pichatu, juzitu lowasa mlikuwa mnamsafisha nakumtandikia makanga chini apite, mmechezeshewa kipanya sasaivi karudi Ccm maisha yanaendelea mmnakodoa mimachotu hamjui mnachotaka.

Kwenye ishu ya Lowasa mngemuwajibisha mtu ndio ningewaamini Nyumbu.
Huna hoja ,na ujinga mtu mzima Kama wewe na jirani yangu kuwa na majungu ya kitoto, Mambo ya kitaasisi Kama chadema kuyazungumzia bado Sana kwako,kajipange upya
 
Wamevuliwa kihalali?

1. Je, walikwenda bungeni kihalali?

2. Kikao gani cha Chadema kilipitisha majina yao?

3. Kiongozi gani wa Chadema alipeleka majina yao tume ya uchaguzi?

4. Je, wamevuliwa uanachama kihalali?

Hayo ndio maswali tuliyopaswa kuyatafutia majibu.

Nasikitika kwamba Watz tumeshindwa kuuliza maswali hayo mawili ya msingi kwa wahusika.

Ningetegemea waandishi nguli kama Pascal Mayalla wangeonyesha mfano kwa waandishi wachanga badala ya kujaribu kupoteza watu wajadili mambo yasiyo na msingi.
 
..huko ni kutokufuata na kuvunja sheria.

..tunaweza kuona hili ni jambo dogo na halina madhara.

..lakini kuna hatari mbele ya safari sheria zikavunjwa kwa mambo makubwa zaidi.
Kama yapi zaidi .?
 
Back
Top Bottom