Halima Mdee: Serikali iache kukimbilia kukopa inadumaza akili

Humu jf Kuna watu kila siku wanaimba Mungu wabariki wazungu kisa wanahudhuria mahakamani.
Sasa mwenzao anaona wazungu siyo wa kutuletea maendeleo.
Chadema hawajielewi.
Lakini si mnasema kuwa Halima ni mbunge wa Chadema? Kama ni hivyo, si anatoa msimamo wa Chadema? Huko kutojielewa kunatoka wapi sasa?

Amandla...
 

Ndio kuna nchi isiyokopa ila inakopesha mfano Saudia Arabia na Qatar na Kuwait na united arab emirates na Brunei wapi walikopa nchi hizi nionyeshe data
 
Mbona yeye mwenyewe kakwopa na CCM kutoka Chadema...
 
Kama tulikuwa tunawaza pamoja
 
Tanzania Kuendelea kukopa Pesa isiyokuwa na Tija haifanyi watanzania kuondokana na Umasikini, Bali mikopo Hiyo isiyokuwa na Tija inaongeza Umasikini kwa Watanzania.

Kwenye Uchumi wa Nchi Yetu, Siasa haitakiwi,
 
Wenye akili hawana uwezo wa kufanya maamuzi halafu wenye uwezo wa kufanya maamuzi kwaajili ya taifa hawa akili. [emoji119][emoji119][emoji119]
 
T350 duh nahisi nimesikia vibaya

Viva Magu Comrade wa kweli
 
..Inabidii iundwe wizara ya kushughulikia mikopo na misaada.
 
Hii serikali ni mikopo, misaada, mikopo, misaada.

Samia anaamini akiwafurahisha wazungu ndio tutatoka kwenye umasikini, kwamba wazungu watatuondoa kwenye umasikini kwa kutukopesha na kutupatia misaada.

Hii nchi kwa kweli alieiroga alishakufa.
 
Which is very true ..mtu mweusi akili yake anajua mzungu ndio atamtoa kwenye umasikini, hamna historia ya namna hiyo, nchi zote zimetoka kwenye umasikini kwa kuwa na mikakati mizuri ya ndani na viongozi wazalendo sio "puppets wa wazungu".
Exactly mikamati ya kutengeneza hela, CEO yeyote lazima uwaambie bodi unampango gani wa kuiongezea kampuni profit tofauti na hapo wanakupiga china

Nchi za kiafrika lazima wafanye kazi kutumia hii mentality kwamba rais useme unampango gani wa kuiongezea revenue kupitia vyanzo tofauti na sio kukopa, au unaweza kopa ili utengeneze ela nyingi Zaid hiyo ya kuwafikia financial freedom lakin kwa hizi mbinu za chief hangaya na viongozi wengi wa kiafrika tutasubiri sana
 
Halima ana haki ya kuongea lakini ukweli ni kwamba Yeye yuko vizuri anafaidi keki ya Taifa.

Leo hii ukitaka kupeleka miradi kwa haraka Ili iwe na tija lazima ukope,na uzuri wa Kukopa unalipa taratibu bila maumivu na Kwa mda mrefu na pia inaweza wewe usilipe wakaja kulipa wengine.

Hii ya eti inalemaza ni kitu kigumu kuelewa inalemazaje wakati unakopa na kulipa.Unaweza kudunduliza kiasi gani hadi ulete maendeleo kwenye Nchi?

Halima anaweza nitajia Nchi yeyote anayoijua yeye ambayo imeendelea bila mikopo? Kama mikopo inalemaza vipi Kuhusu misaada? Bora angesema misaada angeeleweka.

Mwisho ni kwamba Halima anataka Rais asikope Ili alete Kodi za kumwaga kwa wananchi? Kuna uchumi unaweza kujua kwa kuua purchasing power?

Jamani sio kila kenge ni WA kumsikiliza,Rais asiwasikilize Hawa wapuuzi ambao Wanafaidi kodi za maskini,Rais wasikilize wachumi na sio Hawa washenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…