Yego mlaunu
JF-Expert Member
- Jun 12, 2020
- 234
- 269
Halima amesema siyo kila changamoto ni ya kutatua kwa mikopo...Labda kamaanisha mikopo ile ya kujengea madarasa,kwa hakika madarasa tungeweza kujenga kwa pesa za kodi zetu tu.Halima ana haki ya kuongea lakini ukweli ni kwamba Yeye yuko vizuri anafaidi keki ya Taifa.
Leo hii ukitaka kupeleka miradi kwa haraka Ili iwe na tija lazima ukope,na uzuri wa Kukopa unalipa taratibu bila maumivu na Kwa mda mrefu na pia inaweza wewe usilipe wakaja kulipa wengine.
Hii ya eti inalemaza ni kitu kigumu kuelewa inalemazaje wakati unakopa na kulipa.Unaweza kudunduliza kiasi gani hadi ulete maendeleo kwenye Nchi?
Halima anaweza nitajia Nchi yeyote anayoijua yeye ambayo imeendelea bila mikopo? Kama mikopo inalemaza vipi Kuhusu misaada? Bora angesema misaada angeeleweka.
Mwisho ni kwamba Halima anataka Rais asikope Ili alete Kodi za kumwaga kwa wananchi? Kuna uchumi unaweza kujua kwa kuua purchasing power?
Jamani sio kila kenge ni WA kumsikiliza,Rais asiwasikilize Hawa wapuuzi ambao Wanafaidi kodi za maskini,Rais wasikilize wachumi na sio Hawa washenzi.
Halima anaweza kuwa amekosea kwenye maoni yake kimtazamo na ya kwako,ila abadani hajafikia hatua ya kuwa kenge kama unavotaka tuamini