Halima Mdee: Serikali iache kukimbilia kukopa inadumaza akili

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Chadema ameishambulia serikali kwa tabia yake mpya ya kukimbilia kukopa kila kunapotokea changamoto kwani tabia hiyo hudumaza akili na kuuwa uwezo wa kufikiri na kutumia fursa zilizopo ndani ya nchi.

Mdee amebainisha kuwa kwenye report ya CAG imeonyesha kuwa serikali imeshindwa kukusanya zaidi ya trillioni 300 zilizokwama kutokana kesi kushindwa kuamliwa mahakamani.

Cha ajabu badala ya serikali kujikita kuzikwamua hizo hela zilizokwama na kuongeza mapato badala yake wanakimbilia kuomba misaada na kukopa kunakopelekea kuongeza deni la taifa.

Which is very true.. mtu mweusi akili yake anajua mzungu ndio atamtoa kwenye umasikini, hamna historia ya namna hiyo, nchi zote zimetoka kwenye umasikini kwa kuwa na mikakati mizuri ya ndani na viongozi wazalendo sio "puppets wa wazungu".
 
Hivi kuna nchi isiyo kopa kweli, jambo la msingi ni kuona namna bora ya matumizi ya fedha za mikopo ni namna gani zinatumika kama zinafanikisha ujenzi wa miradi na utoaji wa huduma za kumnufaisha mwananchi kuna shida gani au ni mradi tu mbunge wa upinzani uonekane umeongea bungeni.
 
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Chadema ameishambulia serikali kwa tabia yake mpya ya kukimbilia kukopa kila kunapotokea changamoto kwani tabia hiyo hudumaza akili na kuuwa uwezo wa kufikiri na kutumia fursa zilizopo ndani ya nchi.

Mdee amebainisha kuwa kwenye report ya CAG imeonyesha kuwa serikali imeshindwa kukusanya zaidi ya trillioni 300 zilizokwama kutokana kesi kushindwa kuamliwa mahakamani.

Cha ajabu badala ya serikali kujikita kuzikwamua hizo hela zilizokwama na kuongeza mapato badala yake wanakimbilia kuomba misaada na kukopa kunakopelekea kuongeza deni la taifa.

Kwa serikali hii inabidi ajichunge kuhusu neno "serikali kukopa." Linaweza kumtokea puani! Amwulize Ndugai kilimpata nini japokuwa yeye alikuwa anetetea tozo ila akafanya kosa kwa kulinganisha akasema bora tozo kuliko kukopa. Ile kuonyesha kuwa hapendi kukopa kukamkosti!
 
Huyo mdee anataka sisi wananchi tukamuliwe tukondee, huku wao wakijilipa mishahara minono huko bungeni pumbavu Sana....

Mama Samia kaona isiwe kesi, ni kukopa na kufungua nchi Hadi maskini wafaidike kwa namna moja au nyingine
 
Kwa serikali hii inabidi ajichunge kuhusu neno "serikali kukopa." Linaweza kumtokea puani! Amwulize Ndugai kilimpata nini japokuwa yeye alikuwa anetetea tozo ila akafanya kosa kulinganisha kusema bora tozo kuliko kukopa. Ile kuonyesha kuwa hapendi kukopa kukamkosti!

Halima anatafuta sababu ya kutimuliwa bungeni, hiyo meza anayotingisha ina vinywaji vya wakwe.
 
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Chadema ameishambulia serikali kwa tabia yake mpya ya kukimbilia kukopa kila kunapotokea changamoto kwani tabia hiyo hudumaza akili na kuuwa uwezo wa kufikiri na kutumia fursa zilizopo ndani ya nchi.

Mdee amebainisha kuwa kwenye report ya CAG imeonyesha kuwa serikali imeshindwa kukusanya zaidi ya trillioni 300 zilizokwama kutokana kesi kushindwa kuamliwa mahakamani.

Cha ajabu badala ya serikali kujikita kuzikwamua hizo hela zilizokwama na kuongeza mapato badala yake wanakimbilia kuomba misaada na kukopa kunakopelekea kuongeza deni la taifa.

Ubunge wake umeushikilia kwa uzi mwembamba, haya masuala ya kukopa asiyazungumze kabisa muulize Job Ndugai nini kilimtokea.

Nasema tutakopa hata kama ni kujenga nyumba za ma Chief tutakopa.

Ngongo kwasasa Ngorongoro
 
Aliyekuwa spika , Bwana Ndugai; Chagueni moja kati ya Tozo ama mikopo

Rais Samia: Mimi nimechagua Mikopo,, kwani Mimi ndye wa kwanza kukopa? Waliopita hamkuwaona wakikopa?? Tena Bwana Ndugai unikome
Ndugai: Kama mmechagua mikopo basi futeni TOZO za miamala ya simu.
Hangaya: TOZO sifuti na uondoke mara moja kwenye Kiti cha USPIKA
Ndugai: Sawa tutaonana 2025
Hangaya: Hunifanyi lolote
 
Ukiachana na makando kandi mengine Halima Fundi sana nyiee🙌
 
Back
Top Bottom