Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Ukweli ni kwamba Mbowe na Mnyika wanajua wamewasaliti kina Mdee. Mawasiliano ya simu yapo na sauti. Subirini labda wasiende mahakamani.
Ngoja tusubiri Marine azam stand ya Magufuli.

Lets wait!
 
DJ Niletee picha ya Halima Mdee akibusu picha ya hayati.
 
Ukweli ni kwamba Mbowe na Mnyika wanajua wamewasaliti kina Mdee. Mawasiliano ya simu yapo na sauti. Subirini labda wasiende mahakamani.
Mkuuu samahani , unataka kusema hao wabunge 19 akina mdee na wenzake walipewa ruhusa kutoka kwa mbowe na mnyika ,?!?! Na kama ni ivyo hii inawezekanaje ?!
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ndani ya Baraza hilo ni uhuni.




Matokeo ya jumla

Idadi ya wajumbe 423

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%

====

UPDATES ;

=====

Habari zaidi kutoka Gazetini;

Dar es Salaam. Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ni uhuni.

Mdee ambaye amepata kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe na Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Bawacha, ni miongoni mwa makada walifukuzwa baada ya Bazara Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.

Matokeo ya jumla

Idadi ya wajumbe 423

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%

Chanzo: Mwananchi

Vyama viko vingi ,ulitegemea ule pesa au wao Wana njaa wakubaliane na nyie?

Vyama viko vingi hamieni ACT Wazalendo
 
Ni uhuni au ukatili?.

Maana hapa ni kama kukatiwa bomba linaloleta maji nyumbani kwako.
 
Huu uamuzi kama ukifanyika ndio unaenda kuwa mwanzo wa tatizo jingine, hapa zitakuja assumptions za kila aina toka kwa maadui wa Chadema.

Hapa utatumika ukanda, ukabila, mahusiank, dini, na sababu nyingine zote ili kuhalalisha kina Mdee wameonewa ili wawekwe watu wao.

Nawashauri Chadema wabaki na msimamo wao wa mwanzo, kutoyatambua matokeo ya ubunge na Urais wa 2020 na kutopeleka wabunge bungeni, kama shida ni ruzuku, waendelee kuokoteza mitaani kama wanavyofanya.

Kwangu ni bora kupitia machungu ili kulinda heshima, kuliko kubadili msimamo wako na kupata kingi huku ukijipotezea heshima, hapa wasiyumbe kimsimamo.

Hakuna namna wanaweza "substitute" maamuzi yao ya mwanzo kwa kupeleka majina mengine bungeni ikiwa athari za uchaguzi ule bado zipo mpaka leo, hata kama serikali imebadilika.
Hivi umemsikiliza vizuri Mbowe kwenye hotuba yake?

Timu ya watu 10 wa Chadema watakutana na Rais na timu yake, sasa kama Rais mnamtambuwa ni kwa nini wabunge wasiende kuapishwa?

Acheni siasa za itikadi kali mambo yamebadirika na huyu mama ndio Suluhu yenyewe, hii sio awamu ya kuipoteza.
 
Mkuuu samahani , unataka kusema hao wabunge 19 akina mdee na wenzake walipewa ruhusa kutoka kwa mbowe na mnyika ,?!?! Na kama ni ivyo hii inawezekanaje ?!

Ndio utajua maana ya siasa. Mnyika na Mbowe wanajua na ndio waliwaelekeza. Wewe muiteni msajili mahakamni kitalipuka labda waache tu kuweka milage ya Chama kisiasa.
Wengi mnashangaa inakuaje Mdee na uelewa wake aende bila Mbowe kujua.
Ukikurupuka hutaelewa. Tulia utafakari.
 
Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kua watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Hangaya hawezi kuruhusu kurithi maadui wa awamu ya 5,huku maadui hawa wakimharibia ktk uongozi.
 
Mdee na wenzake ni vibaka , piga chini
 
Mkuu, unatakiwa kujua kua mahakama ndie muamuzi wa mwisho kwenye jambo lolote nchi hii.

Kwa hiyo wana haki ya kwenda mahakamani wakitaka. Kumbuka ishu ya Zitto.

Nachokisema, inawezekana mahakama ikakubaliana na uamuzi wa chadema 100% na hilo halina ubishi.

Ila kwa kitendo cha kwenda mahakamani, wanafanya mchezo wa kuchelewesha ama delaying techniques. Kwa hiyo hata Bunge haliwezi kuwafukuza maana bado ni wanachama hadi mahakama itoe majibu, tayari huo muda unakua umeenda na kama ni vikao vya bunge 2 ama 3 wnaakua wamekula hela zetu.

Tusubiri tuangalie.
Kwani sabaya baada ya ile hukumu ya kwanza hakutumikia kifungo hatawakati wa kusikiliza rufaa?Hukumu imetoka,watatumikia mpaka hapo itakapobatilishwa.
 
Hawa wameshajiona kama wamekuwa chama ndani ya chama hakuna mtu atakubali kuwa na kikundi kisichokuwa na nidhamu na kuheshimu uongozi wa juu hakuna anaweza kuvumilia watu wa aina hii kiwe chama chochote au hata kikundi cha kwaya tu huwezi kuvumilia mtu au watu wasiokuwa na nidhamu hata siku moja.
 
Back
Top Bottom