Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Chama ndio rasmi kimegeuka kuwa cha kijeshi. Vyombo vya dola ndio vimebaki pumzi halisi ya ccm. Hata akina januari wanajua fika chama kinatamba sio kwakuwa kuna uwezo wa kushawishi, bali wanajua fika wananchi wanakihofia kwakuwa ukiwapinga unatekwa.
Wananchi wanaipenda CCM hilo halina mjadala!
 
Nyerere alionya kwamba dhambi ya ubaguzi haina mipaka, utabagua watu wa nchi tofauti, utakuja kubagua watu wa kabila tofauti, katika kabila namo utabagua watu wa koo tofauti, mpaka katika familia.

Alitoa onyo hili akiasa dhidi ya dhambi ya ubaguzi. Alitoa mfano wa mifarakano ya Somalia.

Watu wa CCM wamekuwa wakishangilia sana wapinzani wanavyobaguliwa.

Sasa naona kibao kinageuzwa, ukiwacheka hawa leo, kesho kinaweza kuhamia kwako.

Mtu unadukuliwa maongezi yako ya faragha, bila sheria kufuatwa, halafu unalazimishwa kuomba msamaha, unaomba msamaha, halafu unapigwa mkwala wa kuvuliwa uanachama.

Bora hata Memba hajajidhalilisha kuomba msamaha.
 
CCM ni chama makini tofauti na Chadema ambao meya ametaka kutekwa wakawabembeleza watekaji!

Chama makini hakitumii vyombo vya dola na kundi la watu wasiojulikana kupata uungwaji mkono. Ukiona chama kinategemea madaraka ya rais yanayotumika vibaya, ujue hicho sio chama cha siasa, bali kikundi cha kijeshi kinachofanya siasa.
 
Back
Top Bottom