saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 5,673
- 7,811
Nitamshangaa Rais Samia akikubali kugawa eneo lolote la nchi kiutawala, aendelee na msimamo wa mtangulizi wake JPM, Magufuli aliapa asingegawa eneo lolote na akafa na msimamo wake. Kitu muhimu ni kujenga miundo mbinu imara na ya kisasa. Jifunzeni kutoka madiwani wa jiji la Arusha na wa Manispaa ya Moshi wamekuwa wazalendo sana kukataa majimbo yao kugawanywa wapongezwe. Kuhudumia jimbo ni gharama kubwa sana, nchi hii bado ni maskini. Ukitaka kujua umaskini pitia barabara za kutoka Dodoma-Kongwa-Kiteto-kilindi-Handeni, Chukua barabara ya Kiteto-Simanjiro-Arusha, chukua barabara ya Karatu-Mbulu-Haydom-Nduguti-Ibaga-Sibiti-Meatu-Lalago-Kolandoto. Hiyo ni mifano michache, wananchi wa maeneo tajwa hawajui hata matunda ya uhuru wa nchi hii. Watu wa Mbeya walishasahau kuhusu barabara ya lami wao walipendelewa tangia enzi ya mwl. Nyerere. Mh. Rais jenga miundo mbinu ya barabara watu wengine bado wako Tanganyika kabla ya uhuru. Acha kutumikia maslahi binafsi ya wanasiasa, Spika anatakiwa aoneshe mfano kuonesha uzalendo kwa nchi yake. Bahati nzuri km unataka aendelee kuwa spika si lazima awe mbunge km anamhofia Sugu. Hata hivyo nchi hii hakuna mwenye hati miliki usiendeshe nchi kwa maslahi ya watu wachache. Achana na mpango wa kugawa majimbo. Jimbo la Sikonge ni kubwa kuliko baadhi ya mikoa sijasikia mpango wa kuigawa, hapo Mbeya kuna siasa ya hovyo usiwaendekeze