Halmashauri ya jiji la Mbeya jifunzeni kutoka Halmashauri ya jiji la Arusha na Manispaa ya Moshi kukataa jimbo kugawanywa

Kwa nini mbunge anafanya kazi peke yake mkuu?..

Halafu fikiria, mbeya ambalo ni jiji lenye transit ya nchi kibao lakini pia lina shughuli za kutegemewa na nchi kama kilimo. Kwa nini tuwe na wabunge wawili ilhali linatakiwa kuwa ni eneo strategic ambalo serikali inatakiwa kuliangalia kwa potential yake kama ilivyo Dar Es salaam

Sasa kama Mbeya haitazamwi, hapo tatizo ni kukosa mbunge au Mbeya kutokuwekwa kama priority katika mipango ya nchi??...

Kingine kuna mbunge anaepigania Dar kupata flyovers, madaraja na hospital, the same way Dodoma inajengwa kwa sasa?...

Kama jibu sio, je kuongeza mbunge jijini Mbeya kutaleta yote haya kuliko kuishinikiza serikali kuiingiza Mbeya katika mipango yake mikubwa. Na hii haifanywi na mbunge pekee bali policy makers na wadau wa maendeleo kwa ujumla
 
Ilitakiwa wabunge wawe sawa na idadi ya Wilaya 130 over
 
Wanasema baadhi ya majimbo ni makubwa na yana watu wengi kuwahudumia ni shughuli pevu. Majimbo mengine jiografia yake ni ngumu kiutawala kutoka makao makuu ya jimbo
 
Kwanza majimbo yapunguzwe ni mengi sn na viti maalumu vifutwe haraka
Ni majimbo ni mengi sanaaaa mkuu.
Tunatakiwakurudi katika idadi ile ile ya zamani ya wilaya moja mbunge mmoja. Dar es salaam ilikuwa na wabunge watatu tu...,Ilala,Temeke na Kindondoni. Actually, mbunge wa sehemu mojawapo ya hiyo alijua mahitaji ya Dar yote.
Kwa nnavyojua majimbo yalianza kuongezwa kiholela baada ya watu wa mijini kuanza kuamka na kuchagua opposition candidates. Mathalan,
Walipoona jimbo la ubongo ni ngome ya upinzani, wakaanzisha jimbo la Kibamba. Mbunge wa Ubungo anashindaje kuhudumia Kibamba?
 
Nikuongeza gharama za kipumbavu kwa wananchi, ndani ya jimbo kuna DC/DAS/DED wote hao kazi yao nini?
 
Kero za wananchi zile zile kwa wakazi wa wilaya moja na kuzitatua hakuhitaji wabunge wengi bali rasilimali fedha, wataalam na vitendea kazi! Kuongeza wabunge ni kuongeza gharama!
 
Kero za wananchi zile zile kwa wakazi wa wilaya moja na kuzitatua hakuhitaji wabunge wengi bali rasilimali fedha, wataalam na vitendea kazi! Kuongeza wabunge ni kuongeza gharama!
Uko sahihi. Sometimes unaweza kwepa ghalama wakati huohuo kuna wananchi hafikiwi kabisa.

Mimi pia si muumini wa kuwa na wabunge wengi hasa kutokana na mfumo wetu wa malipo kwa ya wabunge. Wananchi wanahitaji kuwakilishwa ipasavyo. Mfano Mbunge mmoja kwa watu 250,000 ni reasonable kabisa kuwasilisha kero zao kwa serikali. Lakini watu 500K+ kuwakilishwa kuwakilishwa na mbunge mmoja ni changamoto.

Shida ya idadi ya wabunge ni malipo yao na huduma zingine ambazo wanapata kutoka kwa wananchi. Unafikiri wabunge wangekuwa wanalipwa 5M per month ingeleta shida?
 
CCM ni janga la taifa
 
Sidhani kama Mbunge husikiliza kero za mtu mmoja mmoja kama daktari anavyohudumia wagonjwa, bali huwa ni kero za jamii husika. Hivyo watu wawe 500K au 20K katika kata kama kero ni barabara Mbunge mmoja anatosha kuisemea na siyo lazima wawe wabunge wawili au zaidi ndiyo isikilizwe!

Kimsingi Bunge letu ni kubwa mno bila sababu linapaswa kupunguzwa na badala yake waongezwe wataalam (watumishi), vitendea kazi na fedha za kutosha kuhudumia wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…