Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Natoa pendekezo kwa halmashauri ya manispaa ya Morogoro iweke lami kwenye barabara hii muhimu, miaka ya zamani old Iringa Road ilikuwa na lami ambayo baadae iliondolewa kutokana na uchakavu badala ya kutengenezwa! Barabara hii kuanzia njiapanda ya SUA kuelekea Magadu hospitali ya jeshi mpaka Mzumbe na kukutana na new Iringa Road iko kwenye hali mbaya sana baada ya lami iliyochakaa kukwanguliwa.
Kutokana na kukwanguliwa huko imebaki na kokoto zilizojishikilia ardhini na kuvifanya vyombo vinavyoitumia kuchakaza magurudumu vipitapo. Kutokana na tatizo hili kunalazimisha magari yanayotokea upande wa SUA kuelekea upande wa Iringa kuenda Msamvu ili waingie barabara mpya ya Iringa hivyo kuongeza wingi wa magari hapo kwenye mzunguruko wa Msamvu kuelekea Dodoma na Dar es Salaam.
Manispaa hainabudi kuitengeneza barabara itakayopunguza magari yatokayo upande wa Iringa kuingia mjini kwa kupitia Mzumbe, Magadu mpaka SUA
Bahati mbaya mbunge wa Morogoro haijui barabara hii inayotumiwa na wagonjwa waendao hosipitali ya jeshi Mzinga.