DOKEZO Halmashauri ya manispaa ya Morogoro wekeni lami barabara ya zamani ya Iringa kuanzia SUA, Magadu mpaka Mzumbe

DOKEZO Halmashauri ya manispaa ya Morogoro wekeni lami barabara ya zamani ya Iringa kuanzia SUA, Magadu mpaka Mzumbe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hivi bara bara zimerudishwa Chini ya Halmashauri kuanzia lini?@moderator hebu fanyeni ile inaitwa fact check
 
Sipendi ujuaji wako, wapi nimebisha? Nimehoji jinsi TARURA wanavyoweza kujua mahitaji ya miundombinu ya barabara za mijini wakati wahusika wakuu ni madiwani.
Sipendi dharau.
Baraza la madiwani wanaingia wadau wote wanaohudumia wananchi na wanajibu maswali yote ambayo yanawahusu!
Awe meneja wa Tanesco, TARURA, RUWASA,TRA, Polisi, etc
Note: kuna Baraza la wazi ambalo hata wananchi wanaruhusiwa kuingia.

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
Hili silo lililoniudhi, sikupenda kauli yako dhidi yangu, hauwezi kuniaminisha kuwa kila nikijuacho wewe unakijua, na si kila ukijuacho lazima mimi nikijue na nisipokijua ninakuwa mpumbavu! Jitafakari.
 
Wakazi wa Morogoro teremkeni huko milimani mje mjini kwani mji wenu kasoro bahari mliokuwa mnajivunia hivi sasa umechakaa umechoka, mmewaachia wageni hawawezi kumkaba mbunge wenu.
 
Kwahiyo manispaa hazisimamii barabara! Hawa madiwani kwenye vikao vyao wanaongelea nini! TARURA nao wana ingia kwenye vikao vya madiwani? Kwakua si madiwani hwawana sifa ya kuingia kwenye hivyo vikao, sasa wanajuaje matatizo ya barabara za mijini?
Ni jukumu la TANROADS na TARURA. Mzumbe ipo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero (Mvomero RC), SUA ipo Morogoro Manispaa (Morogoro MC). Ni mamlaka mbili tofauti. Mvomero DC barabara zake zinasimamiwa na TARURA na Moro MC barabara zake zinasimamiwa na TANROADS
 
Mbona uko hivyo! Hivi uliowataja wanapata wapi taarifa za mahitaji, wananchi tunaandika na mbunge pamoja na wahusika wote akiwemo mama anayetoa hela za ujenzi huku bajeti inayopitishwa na bunge hatujui inapelekwa wapi!
Si jukumu langu kuwaandikia wakurugenzi wa Tarura au Tanroads, ninamwandikia anayekusanya kodi toka kwangu na yeye, mbunge na hao wawili watawasiliana na kushauriana nani atekeleze na uchaguzi uko njiani mama atatoa hela zake kabla ya uchaguzi ajenge.
 
Mmeshindwa kumwajibisha mbunge wenu Abood,huyo ndiyo kikwazo chenu.
Msiendelee kufurahia gari zake za kuwapeleka kwenye mazishi tu.
 
Hivi bara bara zimerudishwa Chini ya Halmashauri kuanzia lini?@moderator hebu fanyeni ile inaitwa fact check
Ni barabara siyo bara bara. Ninalipa kodi kwenye halmashauri ambako wapo madiwani na huko ni rahisi kumpata mbunge kuliko kwenda Tanroads au Tarura ambao sina uhusiano nao na siwachagui na hawana madiwani wa kunisikiliza.
 
Morogoro kwenye barabara hawapo serious,mjini kabisa barabara ni za vumbi,yaani wanashindwa hata na Kahama,mji uliopata hadhi ya manispaa juzi tu
 
Naona kumezuka hoja ya kijinga kuwa niwaandikie Tanroad au Tarura kuhusu barabara hii! Hoja hii sijui imeanza lini na sijui kama madiwani na wabunge wetu wamehamishiwa huko ambako watatusikiliza na kutatua matatizo yetu. Hebu wajuvi nielezeni jinsi hao Tarura na Tanroad wanavyopata taarifa za mahitaji ya ujenzi wa barabara zilizomo ndani ya miji kama hii ya kuanzia SUA kuelekea Mzumbe, kwa waishio Dar ni kama toka chuo cha Ustawi wa Jamii kwenda Mbezi.
 
Sipendi ujuaji wako, wapi nimebisha? Nimehoji jinsi TARURA wanavyoweza kujua mahitaji ya miundombinu ya barabara za mijini wakati wahusika wakuu ni madiwani.
Sipendi dharau.
Na kuongezea hapo,,tarura pia wanawasilisha bajeti yao kwenye Baraza la madiwani,,kwa hiyo hauwezi kutenganisha madiwani na TArura ingawa Tarura hawaripoti kila kila siku kwa madiwani,,ILA BAJETI YA TARURA INAPITISHWA NA MADIWANI
 
Back
Top Bottom