KERO Halmashauri ya Mji wa Mbulu inatunyanyasa Watumishi wake kwa kutunyima haki zetu za msingi

KERO Halmashauri ya Mji wa Mbulu inatunyanyasa Watumishi wake kwa kutunyima haki zetu za msingi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mkoa wa Manyara, tunaomba msaada wenu kufichua changamoto na madai yanayoikabili halmashauri yetu.

Tumekuwa tukikumbwa na uongozi usioridhisha kuanzia ngazi ya madiwani, Mkurugenzi hadi wakuu wa idara mbalimbali. Kwa mtazamo wetu, viongozi hawa hawazingatii ipasavyo maslahi na ustawi wa watumishi, na mazingira ya kazi yamekuwa ya hofu na vitisho.

Baadhi ya watumishi walioajiriwa takribani miaka miwili iliyopita bado hawajalipwa posho za kujikimu. Wanapofuatilia madai yao, hudai wanajibiwa kwa lugha isiyoridhisha au kutishiwa kutothibitishwa kazini au kuhamishiwa maeneo yasiyofaa.

Pia, baadhi ya watumishi wanapangiwa majukumu ambayo hayaendani na taaluma au nafasi walizoajiriwa. Kwa mfano, baadhi ya watendaji wa kata na vijiji hulazimika kufanya kazi za usafi wa jengo la utawala au kushinikizwa kukusanya mapato, licha ya kuwepo kwa watumishi wenye jukumu hilo.

Aidha, tunadai kuwa mazingira ya kazi yanaongozwa kwa vitisho. Wakati mwingine, barua za uhamisho kutoka TAMISEMI hufichwa ili kuwazuia watumishi kuondoka.

Tunaomba mamlaka husika na wadau wa uwajibikaji wachunguze madai haya kwa kina na kuchukua hatua stahiki. Watumishi wengi wamekata tamaa kutokana na hali hii na wanahitaji msaada ili kurejesha mazingira bora ya kazi.
 
Back
Top Bottom