DOKEZO Halmashauri ziangalie Vijana wanaojitolea Vituo vya Afya, wanafanyakazi nzuri lakini wana hali ngumu

DOKEZO Halmashauri ziangalie Vijana wanaojitolea Vituo vya Afya, wanafanyakazi nzuri lakini wana hali ngumu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Dr nsunza

New Member
Joined
Jul 31, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Kuna changamoto kuhusu utekelezaji wa mikataba ya watumishi wa afya chini ya TAMISEMI iliyotolewa mwaka 2025, ambapo baadhi ya watumishi wanalipwa kiasi cha shilingi 100,000 kwa mwezi, huku kukiwa na malalamiko kuhusu kutokuwepo kwa usawa katika malipo ya kazi za ziada (overtime).

Baadhi ya vituo vya afya hulipa watumishi wao malipo ya overtime yanayofikia hadi shilingi 400,000 kwa mtumishi, lakini wafanyakazi wa kujitolea wanapoomba malipo, huambiwa kuwa hakuna fedha.

Pia, kuna malalamiko kuwa baadhi ya watu wanaojiita wasimamizi (supervisors) hulipwa kwa muda wa ziada wanaofanya kazi, huku wengine wakifanya kazi kwa muda mrefu bila malipo yoyote.

Tunaomba halmashauri husika, hasa zile kubwa, ziangalie hali ya vijana wanaojitolea katika vituo vya afya na kutafuta namna ya kuwasaidia. Inadaiwa kuwa baadhi ya halmashauri hulipa angalau nusu ya mshahara kama ilivyoelekezwa na Serikali, huku nyingine zikishindwa kufanya hivyo.

Swali kwa TAMISEMI na halmashauri husika: Ni utaratibu gani unaotumika kuhakikisha malipo ya watumishi wa afya na wale wa kujitolea yanakuwa ya haki na uwazi? Tunaomba suala hili lifanyiwe kazi ili vijana wanaotoa huduma katika vituo vya afya wasiendelee kufanya kazi katika mazingira yenye changamoto za malipo.
 
Back
Top Bottom