Mkuu hauendi na updates za vita hii'nini?
Mwenzako yupo sahihi, hao raia millioni 1.5 ni pamoja na wakimbizi kutoka upande wa kaskazini ilipoanzia ground attack.
Huko nako walianza kwa kutangaziwa hivi hivi kuhama kwa ma loud speaker, tena wakaelekezwa na pa kwenda kabisa ndiyo huko Arafah.
Wote waliokaidi na kukomaza mafuvu walichinjwa.
Israel haivamii kisiri, inaanza kwanza kutangazia raia kuondoka kisha ndiyo inavamia na kukalia maeneo, wanaokutwa hawajaondoka, jamaa wanahesabu ni halali yao.
Kusema watakwenda wapi, adui haulizwi aina hiyo ya swali, maana majibuya mahali pa kwenda huwa wanayapata bila kufundishwa.