Kwa hiki kipande tu nimekuona hauna akili kabisa. Kwa akili yako unadhani bado kuna sadaka za kutekezwa siku hizi? Kwamba Mungu anapokea sadaka za kuchinjwa? Kwa kuhani yupi sasa?
Acheni upotoshaji nyie wasabato, kama mnadhani ufunuo upo direct hivyo basi tusubiri pia vita vya kutumia farasi na mapanga maana ndio ipo kwenye ufunuo ilihali kuna vifaru na bunduki siku hizi!!
Huna akili wewe ,ndio maana nilishakupuuza ,ila kwakuwa akili yako finyu basi ukiniona unawashwa ,
Kwanza, Hoja kuu siyo kama Mungu anapokea sadaka leo, bali ni mpango wa Wayahudi, si wa Mungu.
Unaposema Mungu hataki tena sadaka za kuteketezwa umekosa hoja, kwa sababu Wayahudi hawamngojei Yesu, wanangojea Masihi wao.
Jitahidi uwe na exposure ujue kuhusu wayahudi,acha chuki dhidi ya wayahudi haitakusaidia kitu,
Ngoja nikupe shule ya bure,
Wayahudi wao wanaamini kabisa kwamba sadaka lazima zirudi mara tu hekalu litakapojengwa tena.
Hii ni imani ya Kiyahudi, si ya Kikristo.
Na ushahidi upo
Daniel 9:27
“Naye ataongeza agano imara kwa wengi kwa muda wa juma moja; na katika nusu ya juma ataikomesha sadaka na dhabihu…”
Hapa Daniel anasema sadaka zitakuwepo tena, kisha zitaikomesha baada ya muda fulani (wakati wa Mpinga Kristo).
Kwa hiyo, Biblia inasema sadaka zitarudi, lakini kwa makosa, si kwa mapenzi ya Mungu ndio maana zikomezwe tena.
Kuhusu Ng’ombe mwekundu (Red Heifer), Hii siyo hadithi ya “WASABATO” acha chuki kijana na wasabato, walikufanya nini?🤣🤣
Huo ni mpango halisi unaoendelea Israel leo.
Kuna taasisi inaitwa The Temple Institute huko Jerusalem, ambayo imeandaa kila kitu cha hekalu la tatu , mavazi ya makuhani, vyombo vya dhahabu, na sasa wanalea ng’ombe wekundu waliotoka Texas, USA mwaka 2022.
Wewe unashinda unakula nguruwe utajulia wapi haya ?🤣
Kulingana na Hesabu 19:1–10, ili kuhani aweze kutakaswa kwa huduma ya hekalu, lazima majivu ya ng’ombe mwekundu yachanganywe na maji ya utakaso.
Hivyo, bila hao ng’ombe, hekalu haliwezi kuanza kufanya ibada.
Na leo hii, majira ya Pasaka 2025–2026, taasisi hiyo imetangaza kuwa watafanya ibada ya utakaso ya kuhani kwa kutumia ng’ombe mwekundu huko Mount of Olives (mlima wa Mizeituni) kwa maandalizi ya hekalu.
(chanzo: The Temple Institute official updates, 2024–2025).
Nakupa hii shule ,maana wewe ni mjinga
Kwa hiyo si hadithi, ni matukio ya sasa.
Kuhusu Hekalu la Tatu ,kosome Biblia na Unabii,tatizo mmezoea kucheza mayenu na ndombolo makanisani ,
Biblia inaonyesha wazi kwamba hekalu litajengwa tena kabla ya ujio wa Yesu.
2 Wathesalonike 2:3–4
“...yule mtu wa kuasi... atakayekaa katika hekalu la Mungu, akijionyesha kwamba yeye ndiye Mungu.”
Kwa hiyo hekalu lazima liwepo ili huyo “mwanamume wa kuasi” (Mpinga Kristo) akae humo.
Hili halijawahi kutokea tangu hekalu la pili lianguke mwaka 70 BK.
Kwa hiyo wanapanga kulijenga tena si kwa mapenzi ya Mungu, bali kwa mpango wa dunia kuelekea unabii wa mwisho.