Nimesoma huo mpango wa point 21 wa kuleta amani Palestina naona ni kama mtego kuwaachia mateka na kujisalimisha rasmi katika utawala wa kimabavu wa Israel.
Eti Baraza la amani la mpito la Palestina litaongozwa na Trump na Tony Blair.
Wapiganaji wa Hamas waweke silaha chini na kuwaachia mateka wote mara Moja na waondoke Gaza
Majeshi ya Israel yataendelea kulinda eneo la Gaza na West Bank na yataondoka taratibu.
Kwa ufupi point hizo chache hapo juu nimeziona kama ni kiini macho tu na Leo la marekani na Israel ni kuachiliwa mateka tu na baada ya hapo wataendelea na vita. Mimi ningekua mmoja wa viongozi wa Hamas ningeupuuzilia mbali mpango huo wa kumpelekea kwenye ukoloni Karne ya 21.
Wapalestina kwa sasa hawana cha kumpoteza kama kufa wameshakufa sana wamalizie tu ngwe iliyobaki kama ni kufa wote wafe waishe ijulikane ( jambo ambalo haliwezekani)
Hivi sasa Israel ana presha kubwa ndani na nje juu ya kutambuliwa kwa taifa la Palestine, hali ya mateka wa Israel huko Gaza, isolation kutoka kwa nchi za ulaya na makundi ya misaada ya kibinadamu hasa kutoka ulaya. Huu mpango wa trump ni kutaka kuzuia hii presha Hamas msikubali.