Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ikiwa ni zaidi ya mwezi sasa tangu vita vianze na huku jeshi la Israel likisema limeizingira Gaza yote kwa vifaru na kubomoa mahandaki yanayotumiwa na Hamas,ghafla leo kombora zito la masafa marefu limeonekana likipaa kutoka Gaza.
Kwa mujibu muandishi wa Aljazeera aliyeko Palestina ya ukiongo wa mashariki,kombora hilo ambalo jina lakie halisi halijajulikana lilifanikiwa kutua mpaka mji wa pembezoni mwa Tel AVIV bila kipingamizi chochote kutoka kwa Iron Dome.
Ufuatiliaji uliofanyika baada ya kutua kwa kombora hilo ulidhihirisha mtaa mzima ukitaharuki huku magari na majumba yakiwaka moto.
Kwa upande mwengine msemaji wa Hamas wa kundi la kijeshi la Alqassan.injinia Osama Hamdan ameilaumu Israel kwa kutokuwa na nia thabitii ya kupatikana mateka inaowashikilia wakiwa hai.
Osama amesema mara kahdaa wameitaka Israel isitishe vita kwa muda ili iweze kuwakushanya mateka 70 wa mwanzo wakiwemo raia wa kigeni ili na nchi hiyo iachie baadhi ya wafungwa wa kipalestina kwenye magereza yake. Sharti lao jengine ni kuruhusiwa misaada iingie maeneo yote ya Gaza bila ubaguzi wa kimaeneo.
Kwa mujibu wa msemaji huyo pendekezo lake hilo limeendelea kukataliwa na Israel kutokana na kiburi chake.