Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Hiyo kumsema kutokana na matendo yake ndiyo bullying yenyewe.Watu wanamsema kutokana na matendo yake ila yeye ndio anageuza maana kuwa eti Wana mbully
Kwa sababu matendo yake, maisha yake, unamsema nini sasa?
Tanzania watu wengi hawajui uhuru wa mtu binafsi, wanajiona wana haki ya kumuingilia mtu katika maisha yake binafsi.
Yani ni hivi, hata Hamisa akiwa anadanga mitandaoni, hayo ni maisha yake. Kama wewe hupendi kudanga kataa kudanga, fundisha watoto wako kudanga ni kubaya. Usifiatilie watu wanaodanga, fuatilia watu wenye falsafa kama zako katika maisha.
Mimi mbona simfuatilii Hamisa na wala sijui habari zake mpaka mzilete hapa JF?
Hamisa akidanga kivyake na mimi nikimuona huyu masikini limbukeni tu nikawa sifuatilii habari zake nafuatilia biashara zangu, nitapungukiwa nini?
Tena nikisikia habari zake naweza hata kumuonea huruma huyu mwanamke hajasoma, katoka familia masikini pengine, mifumo ya nchi yetu imemuangusha sasa hivi ana hustle kudanga tu.
Watu wengi wanaomfuatilia hivyo na kum cyberbully Hamisa hawana life. Mtu mwenye busy life hawezi kumfuatilia Hamisa hivyo.
Atafuatilia mikataba ya biashara, kesi za real estate, investment strategy, trust fund ya familia.
Sasa Wabongo wengi hawana elimu, hawana utashi, hawana kazi. Hawana biashara.
Wangapi wana trust funds za familia hapa? Tunahesabika.
Ndiyo maana kumfuatilia Hamisa imegeuka kuwa kazi yao.