Kuna clip nimeona wakina mama waswahili wanamuogesha mwenzao stendi Mbagala ili kumuondolea mikosi aweze kudumu kwenye ndoa, watu kama hao wanawezaje kuacha kufuatilia wanawake wenzao mtandaoni na kufanya bullying?!
Kuna wanaojiita wasanii na celebrities wanaonyesha kuwa na maisha ya gharama sana mjini wakionyesha majumba na magari ya kifahari halafu wakiumwa wanaomba kuchangiwa pesa tena na umma, Hawa wanawezaje kuepuka cyber trolling?!
Wanaweza kuepuka kwa kujifunza na kujiongeza.
Dunia nzima hata hizi jamii tunazoona zimeweza kuendelea socially, kuelimika etc, wote walikuwa washamba hivyo hivyo.
Ila waliamua kubadilika, wakaamua kuweka juhudi, wakaamua kujifunza, wakafanya kazi, wakabadilika.
Sisi hatujaamua.
Ndiyo maana tumesaidiwa sana kwa miaka yote hii tangu uhuru, na bado ujinga mwingi.
You can take a cow to the river, but you can't force it to drink water.
Sisi wengi tumepelekwa mpaka mtoni, wengi hatutaki kunywa hayo maji.
Halafu wabongo wengi bado wana kiburi cha masikini jeuri cha ujamaa. Yani tunaona hatutaki kuijua dunia, hatutaki kujifunza Kiingereza. Yani hata yale mambo ambayo wengi wanaona hawawezi, si kweli kuwa hawawezi, deep down hawataki, hawajaweka juhudi za kutosha.
Ndiyo maana akitokea mtu mmoja akaweka juhudi akapata scholarship, watu wanashangaa, huyu kawezaje?
Kumbe scholarships zipo tu, watu hawafuatilii.
Mimi kuna dogo alikuja Marekani kapata Scholarship. Nikamualika kwangu akae weekend nimtembeze aione Marekani.
Nilimuuliza umepataje scholarship? Nikafikiri kaunganishiwa kwa family network. Akasema aliiona Twitter akaifuatilia akapata.
Sasa hapo ndipo unaona tofauti ya watu.
Mwingine anafuatilia scholarship ya kuja kusoma Marekani, mwingine anafuatilia maisha ya Hamisa Mobeto.
Mtandao mmoja huo huo wa Internet.
Na si lazima iwe scholarship, kwa sababu si lazima kila mtu aende shule, kuna fursa za mikopo nafuu kibao kwa wafanyabiashara ndogondogo. Nyingine watu wanaangalia business plan yako tu, wanakuchangia hizi $10,000 mpaka $100,000 watu wanachukua tu.
Ila wabongo wanaanzia wapi wakati hata Kiingereza cha business wengi mgogoro?