Hamna mtu mwenye tatoo mwenye tabia nzuri

Ujinga wako kichwani hauhusiani na tatoo
 
Imeandikwa wapi hii? Tupe reference acha blah blah..Au unatoa kwenye fuvu lako?
 
Nawajua wana vitengo kadhaa tena PSU na wanazo na issue zao ni ganja tu hata pombe hawatumii na suti mnawaona.. ni urembo tu kama kupaka piko kwa madem!
PSU ni migambo tu, kuna vitengo vya intelligence lakini sio PSU.
 
Kazi ya maajenti wa shetani ni kutetea kila ushetani na kuupambania uonekane kuwa halali
 
Hakuna wasio na tattoo wenye tabia mbaya over mbwa?
Halafu huyo anayesema tattoo ni mbaya kaambiwa mbona Messi anazo kwa kua anampenda akajibu Messi atolewe kwenye list ya vijana wa hovyo[emoji16]
Hii sasa ndio uhalisia wa Mwafrika kama kitu hakifanyi ni dhambi kama kitu anakifanya au anafanya ampendae sio dhambi,

Amri 10 za Mungu zimeelezea kila kitu na wengi wanadondokea humo lakini hakuna katazo la Tattoo kwenye hizo amri 10 isipokua kuna kimstari fulani kwenye hicho kitabu, basi nakwambia kimechukuliwa hicho kimstari kinatembezwa kila kona na zile amri 10 zimefichwa mbali ili kila mtu ajihisi ni mtakatifu,
Ilhali akikaa mwenyewe anaelewa madhambi aliyoyafanya ya siri na dhahiri, anakosa kujiuliza nani amemuhukumu hadi yeye ajipe kibali cha kuhukumu wengine.
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Kama ni kuvamiwa na roho wachafu anakuwa kashavamiwa tayari. Kujichora tattoo ni miongoni mwa udhihirisho wa kilichopo ndani yake.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Majeshi yapi unayaongelea, haya ya kwetu huku, mbona wajeshi ni walevi , wazinzi, wagomvi na makero kibao na wote hawana Tatoo… VP nidhamu ya jeshi letu ni sawa na USA ambako wanajeshi wake wanaweza kuwa na tatoo bila shida yeyote?

Tabia zipo kwenye fikra, ngozi haina uhusika zaidi ya hisia kupelekwa kwenye ubongo… fake news, fake lesson, fake pastor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…