Hamna mtu mwenye tatoo mwenye tabia nzuri

Hamna mtu mwenye tatoo mwenye tabia nzuri

Bro, mimi baada ya kumaliza form four, enzi zile likizo ya Mkapa, nikachora tatoo, kabla ya hapo nilikuwa mtoto mzuri kabisa, ila baada ya matatoo,

Nikajikuta sitaki tena kushiriki ibada, nikawa kampani yangu masela, nilianza kujifunza sigara, kisha nikarukia kwenye bangi, baadae nikapotea kabisa.

Mwenendo wangu ukapotea na sikuweza kuendelea tena na masomo.

Baada ya miaka mingi kupita ndio nimeweza kurudi kwenye mstari, baada ya mateso makubwa na kupita the most difficult and hard way
Ujinga wako kichwani hauhusiani na tatoo
 
Hii kitu uliyoandika wengi hawaielewi ila ukweli ni kwamba ukishachora tatoo mwili wako unakuwa wazi (exposed) kuingiwa na roho chafu na mambo yote mabaya yatakuhusu iwe physically au spiritually kwasababu kitendo cha kuchora tatoo tayari mwili wako umeshakuwa ubao wa matangazo kwenye ulimwengu wa giza.. no way to escape utaishi kwa utatanishi sana..
Imeandikwa wapi hii? Tupe reference acha blah blah..Au unatoa kwenye fuvu lako?
 
Screenshot_20230113-045646_1.jpg


Screenshot_20230113-045710_1.jpg


Screenshot_20230113-045807_1.jpg


Screenshot_20230113-051622_1.jpg


Tattoo haina shida yoyote na maisha yako, wewe kama unafeli au hutoboi ni kwasababu hufati principal za success. Mambo ya roho sijui nini ni uzwazwa tu
 
Nawajua wana vitengo kadhaa tena PSU na wanazo na issue zao ni ganja tu hata pombe hawatumii na suti mnawaona..
emoji23.png
emoji23.png
ni urembo tu kama kupaka piko kwa madem!
PSU ni migambo tu, kuna vitengo vya intelligence lakini sio PSU.
 
Wewe hayo ni matatizo yako binafsi na kilichokukuta wewe hakiwezi kwa standard unit kwa wote waliochora tatoo, haya Messi baada ya kuchora tattoo alikuwa mtoto mbaya kama wewe?

Watu wote waliochora tattoo wana maisha mabaya kama yako? Kwanini hizo shida uzihusishe na tattoo?

Ninachokiona hapa ni wewe kutafuta justifications juu ya failures zako za kimaisha.

Halafu waafrika tuna mambo ya ajabu sana, kila kitu tunakifikiria kivyetuvyetu tu, tattoo ikuharibie maisha??[emoji23][emoji23][emoji23]
Kazi ya maajenti wa shetani ni kutetea kila ushetani na kuupambania uonekane kuwa halali
 
Hakuna wasio na tattoo wenye tabia mbaya over mbwa?
Halafu huyo anayesema tattoo ni mbaya kaambiwa mbona Messi anazo kwa kua anampenda akajibu Messi atolewe kwenye list ya vijana wa hovyo[emoji16]
Hii sasa ndio uhalisia wa Mwafrika kama kitu hakifanyi ni dhambi kama kitu anakifanya au anafanya ampendae sio dhambi,

Amri 10 za Mungu zimeelezea kila kitu na wengi wanadondokea humo lakini hakuna katazo la Tattoo kwenye hizo amri 10 isipokua kuna kimstari fulani kwenye hicho kitabu, basi nakwambia kimechukuliwa hicho kimstari kinatembezwa kila kona na zile amri 10 zimefichwa mbali ili kila mtu ajihisi ni mtakatifu,
Ilhali akikaa mwenyewe anaelewa madhambi aliyoyafanya ya siri na dhahiri, anakosa kujiuliza nani amemuhukumu hadi yeye ajipe kibali cha kuhukumu wengine.
 
Kwanini huwezi kujiunga na majeshi kama una tatoo? Kwanini huwezi kujiunga na upadre au uchungaji kama una tatoo?

Tatoo zinavuta nguvu hasi (negative energy) yaani hata kama ulikuwa mwema sana kabla hujachora, ukichora utajikuta tu unapata hamu ya kufanya mambo mabaya.

Mabinti wengi wenye tatoo hawaithamini tena miili yao, ndio maana wako tayari kufanywa popote ili mradi tu wapate pesa.

Wengi baada ya kuchora tatoo wakajikuta wana hamu ya bangi, sigara na madawa ya kulevya.

Hata Mungu mwenyewe ndio maana alikataza kuchora tatoos.

Law 19:28 SUV​

Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Kama ni kuvamiwa na roho wachafu anakuwa kashavamiwa tayari. Kujichora tattoo ni miongoni mwa udhihirisho wa kilichopo ndani yake.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Majeshi yapi unayaongelea, haya ya kwetu huku, mbona wajeshi ni walevi , wazinzi, wagomvi na makero kibao na wote hawana Tatoo… VP nidhamu ya jeshi letu ni sawa na USA ambako wanajeshi wake wanaweza kuwa na tatoo bila shida yeyote?

Tabia zipo kwenye fikra, ngozi haina uhusika zaidi ya hisia kupelekwa kwenye ubongo… fake news, fake lesson, fake pastor.
 
Back
Top Bottom