jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Hizi dini zilekebishwe ziendane na mazingira ya sasa na mahitaji ya wakati huu kulingana najamii husika.
Sijajua ni kwanini Wakristo wamekuwa wakisadikishwa na kuaminishwa na wao haraka haraka huamini na mwishowa siku hujikuta wakiwa mateka wa kifikra.
Visa vingi sana tumeviona na tumevishuhudia vya watu kuuziwa kijifuko cha chumvi tu hii ya dukani kwa shilingi laki moja huku wakisadikishwa kuwa inaleta utajiri na kumfukuzia mbali pepo mchafu alitaye ufukara.
Tumeona watu wakisadikishwa kuwa ukipada mbegu utacuna lolote ulitakalo, mathalani, unataka kuwa Mkurugenzi wa bandari, au unataka kuwa daktari mkuu na wewe elimu yako ulikomea darasa la nne A, basi panda mbegu,inenee na wewe utavuna jambo ulitakalo.
Wakristo wameaminishwa kuwa kina St. John, St. Peters, St. Richard na wazungu wengine waliokufa zamani ndio wanaweza kutuombea.
Mizimu ya kizungu, wala haikujui je inawezaje kukuombea? Mizimu ambayo haina hata uhusiano na wewe?
Omba kupitia mizimu ya kwenu, achana na hao wahuni wa kimagharibi, wanachotaka kutoka kwako ni sadaka tu.
Wanahubiri upendo na hawana upendo, hata marehemu Benjamin Williams Mkapa alichana na upadre baada ya kuona huko kwenye mission kumejaa gjiriba, chuki , ubaguzi na upendo haukuwepo.
Mapadre wazungu walikuwa wakiwanyanyapaa na kuwaona mapadre weusi kama takataka halafu wakipanda madhanahuni wanajidai wanahubiri upendo.
Hizi dini zichunguzeni kwa kina, kisha zirekebiswe huenda zikawa bora kidogo
Kingine ukristo ni dini ya upendo na amani..kila mtu amepewa free will mana tumepewa nja mbili ya uzima na upotevuni..kila kitu kimewekwa wazi ni uchaguzi huru.
Tofauti na dini nyingine zimejaa chuki..fitina mauaji..utengano husuda kwa waumini wake wanaofunguka akili ili kutoka vifungoni..kwa kutishiwa uhai na kutengwa na watu wao..kulazimisha wengine wajiunge dini yao wakikataa ni kuuwawa..absurd.
Mungu ubariki ukristo..dunia ni sehemu salama sana chini ya ukristo.
#MaendeleoHayanaChama