Sikiliza Chizi, ilo jina sijui kama utanielewa any way, sisi waisalmu tunakatazwa na Allah kupitia kwa Mtume wake Mwarabu aitwae Muhammad swalallahu Alaih waalih wasallam. Kwa hiyo kwa hili ni kosa kupaeana mikono na mwanamke. waziri huyu yupo sawa kabisa kwa 100%.Kwani nani kasema ni kosa? Mi sijaona kama ni kosa. Hata angekataa mkono wa mwanamke wa Kikristo siyo kosa ni maamuzi. Mimi binafsi sikumbatiani na mwanamke asiye wangu. Ni maamuzi yangu tu. Hakuna aliyenikataza. Ni kama mtu anaamua kuchagua dhambi flani mbaya nyingine nzuri.
Soma hii hadithi;
Imesimuliwa kutoka kwa Ma’qil ibn Yaassar ambaye amesema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake)) [At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]
Jambo hili limekuwa ni mazoea katika jamii yetu na linaonekana ni jambo la kawaida na kuliacha huwa ni kama muhali kwa mtu kukhofu kuwa atakuwa amemdharau mwanamke asipopokea mkono wake anaposalimia. Inampasa Muislamu aondoshe fikra hii ambayo ni wasiwasi wa Shaytwaan na abakie thabiti katika Iymaan yake ya utiifu wa amri wa Mola wake na asione aibu kwani Allaah Haoni aibu katika haki.