Hizi ni propaganda nisizokuwa na muda nazo kabisa.
Samia akitaka kuwa kiongozi mzuri wa nchi hii, asimamie serikali yake na watendaji wake watimize wajibu wao kwa wananchi.
Afanye kazi na waTanzania zaidi kuliko kudhani waTazania hawawezi kufanya kazi kwa ufanisi.
Aaachane na hii tabia ya kufanya mambo kiujanja ujanja na hadaa. WaTanzania ni watu waelewa sana; wanapoona hila wanazitambua kuwa ni hila.
Wewe usidhani waTanzania hawakuelewa Magufuli alikuwa akifanya nini, pamoja na ukichaa wake mwingi aliokuwa akiuonyesha mara kwa mara.
Kama wewe unadhani Samia haleti uharibifu mkubwa katika anayoyafanya sasa, kuliko alivyokuwa akifanya Magufuli, waTanzania wanaelewa ni nani mwenye madhara makubwa kwa nchi yetu, kati ya Magufuli na Samia.
Kwa hiyo usije hapa na vitisho vya Magufuli, na kusifu umalaika wa Samia.