Mi sio bogus fan ambae anaamini kila kitu anachosema mzee muddy ni sahihi...siwez kua hohehahe kama nyie maalim muddy company ..nacriticize napoona panafaa kua criticized..pia mdhani sisi tunamuabudu Nyerere hapana Sidhani kuna kumuabudu Nyerere bali ni ile heshima kama muasisi wa Taifa kama alivyo Karume muasisi kule Zanzibar.Tusiwe tu wa kupinga ukweli Tupende tusipende atabakia kama kiongozi maarufu na Mwenye mchango mkubwa sana African hata kama kuna WATANZANIA kina mzee Ms mtalazimisha kumfuta !!! Uzuri historia imeshaandikwa na hata wanaojaribu "kusahihisha" kwa kumpaka matope na kumchafua hawataenda mbali sana zaidi ya kwenye vijiwe kawaha na Samaki lkn sisi tunakubali makosa kadha wa kadha ya kihistoria ya Nyerere ambayo hayahitaji weledi wa juu kuyaona. Upande wenu hata hivyo, hamko tayari hata kukiri zuri moja la Nyerere na hivyo mnajitahidi sana kumfanya Shetani. Itawasaidia mkijaribu japo kidogo kutambua mchango wa Nyerere kwa maisha, fikra na historia ya Tanzania - labda hapo mtakuja kwenye kuhumu kwa mizani ya haki kidogo. Katika hili tunaomtetea ukweli wa Nyerere tunawapita sisi wengine tupo kuweka rekodi sawa ili wasomao kwa ufahamu wasisumbuke wala wasijekula sumu kila la kheri endeleza Udini wako na company yako
Wembee,
Mchango wa
Nyerere katika TANU na kudai uhuru ni mkubwa sana.
Ikiwa nitajaribu kusema kuwa
Nyerere hakuwa lolote katika historia ya
Tanganyika nitakuwa nimejivunjia heshima yangu.
Ukisoma kitabu changu utakuta sehemu nyingi ambazo zinaeleza vipi
Nyerere alijenga matumaini ya Watanganyika katika kurejesha utu na
heshima yao.
Ila hutomsoma peke yake.
Ikiwa ni katika mikutano ya mwanzo 1955 pale Mnazi Mmoja utamsoma
Nyerere,
Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Titi Mohamed na wengineo.
Ikiwa safari ya kwenda UNO utamsoma
Nyerere na
Idd Faizi Mafongo,
Mwalimu Kihere na wengineo.
Ikiwa sakata la kura tatu utamsoma
Nyerere na
Sheikh Rashid Sembe
na
Hamisi Heri na wengineo.
Hutomsoma
Nyerere peke yake.
Utakapokuja katika kuasisi TANU utasoma nimeandika historia ya TANU ni
historia ya maisha ya
Abdul Sykes na katika maisha hayo pia utamkuta
Julius Nyerere,
Hamza Mwapachu na wengineo.
Hapa ndipo ilipo tofauti baina yako na mimi.
Ikiwa wewe utaona huu ni udini hii ni bahati mbaya kwa upande wako.
Nasema ni bahati mbaya kwa sababu kitabu changu kimefanyiwa ''review,''na
mabingwa wa historia ya Afrika duniani kama
John Iliffe, James Brenan,
Jonathon Glassman na wengineo.
Hili la udini hakuna hata mmoja ameliona isizidi ndiyo ikawa sababu ya mimi
kualikwa kwenye vyuo vyao kuzungumza.
Hakuna alomfuta
Nyerere katika historia ya TANU lakini wapo waliomfuta
Abdul Sykes katika historia ya TANU na
Nyerere alikaa kimya.
Ikiwa unadhani historia ya TANU na historia ya
Nyerere imeandikwa basi
nakuhakikishia historia hiyo ndiyo sasa inaandikwa.
Chanzo cha kuiandika historia hii ni mazungumzo kati ya
Prof. Haroub
Othman na
Nyerere, Prof. Haroub alipomwambia
Nyerere, ''
Mwalimu
lazima uwajibu
Ali Muhsin na
Mohamed Said.''
Majibu ni kwa ajili ya vitabu walivyoandika
Ali Muhsin na
Mohamed Said:
Wembee,
Soma vitabu hivi utakudhihirikia kweli kuwa historia ya Tanganyika
ilikuwa bado haijaandikwa.
Hao maprofesa unaowaona hapo chini ndiyo sasa wanaandika historia
ya
Mwalimu Nyerere ambayo ndiyo historia ya TANU na historia ya uhuru
wa Tanganyika:
Prof. Saida Othman na Prof. Issa Shivji aliyekaa chini ni Mwandishi katika mahojiano
kuhusu Mwalimu Nyerere na TANU nyumbani kwa mwandishi.