Ndugu sio kila anachokisema mtu mwenye wadhifa fulani eti ndiyo itakuhakikishia kuwa ameongea kitu sahihi na kupuuza maoni ya mtu asiye na wadhifa. Tambua kuna watu hawana ujasiri wa kupinga ili kutetea nafasi zao japo ukweli wanaujua.
Kwahiyo kabla ya kuongea, kufanya au kukubaliana na jambo fulani, jipe nafasi ya kufanya uchambuzi wa kina na sio kuelea au kukubaliana moja kwa moja eti kwakuwa tu jambo hilo kasema msomi fulani, kiongozi fulani au mwanafalsafa fulani.
Sent from my TECNO KC6 using
JamiiForums mobile app