Hanspaul: Mshahara wa Laki 5 usikatwe Kodi


Anachomaanisha ni ukiongeza uwezo wa manunuzi wa raia wako wigo wa kodi unatanuka mno, unachohitaji ni mifumo ya urasimishaji na ukusanyaji. Amewaza vizuri.
 
Itazame kwa jicho la macro siyo micro.
 
Kinyume chake pia ni sawa.
Kinyume chake hata akiitumia kama ulivyosema, still kwa kuongeza uwezo wa spending wa raia wako utatanua mno wigo wa kodi sababu kodi inatokana na biashara, na kwenye kila biashara kuna matumizi na wasababisha matumizi ni waajiriwa na waajiriwa wengi wanalipwa laki saba mpaka tano kabla ya kodi.

YAANI KWA UFUPI, HUYU ANASHAURI WAAJIRIWA WALIO WENGI WAWE NA PESA ILI WAKASPEND KWA WAFANYABIASHARA, WAJENZI N.K MAANA NDIO KUNDI KUBWA.
 
Angeshauri kuwa kima cha chini kiwe 500,000/- ambayo haikatwi kodi. Hapo angeongeza hio spending power.
Ila ya kusema tu chini ya 500,000 isikatwe kodi hawatamuingezea mwananchi chochote ila wao matajiri wataokoa hela zao maana wataendelea kulipa watu wengi 270,000 bila kulipa PAYE.
Point yako nimeielewa vizuri pia.
 
Upo sawa Mkuu RRONDO
 
Means serikali pia pia ipunguze unnecessary spending.
Magari ya 500b kila mwaka ilhali tunaagiza mafuta ya kupikia yenye thamani ya 500b..kwanni tusiwekeze kwa watu wetu kwenye kilimo cha kisasa kupungiza umasikini,kuongeza ajira na kupandisha thamani ya sh?
Kuna baadhi ya vitu unaona kabisa ni ubinafsi!
 
 
Na kwa serikalini mshahara chini ya laki nane kodi ipunguzwe
 
Lengo la Mkurugenzi ni kuongeza uwezo wa wananchi kununua vitu ambavyo, kiuhalisia vitu wanavyo nunua vinakua vimesha katwa kodi, kwa kifupi ana maanisha serikali iache double taxation.
 
nimewaza kama wewe ulivyowaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…