Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Maisha hayana formula, wewe pambana tu huenda kesho ikawa zamu yako
Japo siyo kazi rahisi coz Kila njia ina miiba
 
Kawaida ya binadamu tuna hulka ya kutamani tusichokuwa nacho.

Umasikini ni kitu kibaya sana kakini kwenye maisha Amani ya Nafsi ni bora kuliko chochote.

Magufuli alikuwa anapenda kwenda kwake CHATO mara kibao ingawa angeweza kuishi Osterbay, Ikulu.

Prod Mwandosya kaamua kukaa kwake huko Mbeya ingawa anaweza kuishi Masaki.

Jambo la msingi ni kuishi sehemu inayokupa Amani.

Na watu wengine pia wanapenda kuishi na watu wanaofahamiana nao ( kijamaa ) maana wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha, siyo kama Osterbay kila mtu ndani ya geti zito lenye umeme.

Leo kina Akon wametafuta pesa US lakini wamerudi Senegal ambako wanaheshimika zaidi.
 
Niliwahi kusikia kwamba ilikuwepo hata miaka ya karibuni inayofanywa na watu binafsi. Magari yao yako wazi kabisa kule nyuma ni Malori ya kawaida tu. Sasa kama kuna upepo uchafu wote hupeperushwa mitaani na kufanya uchafuzi mkubwa sana.
Zamani miaka ya themanini nakumbuka Upanga magari ya Halmashauri ya Jiji Dar es salaam yalikuwa yanazunguka kuzoa uchafu. Kila wiki gari la jiji linakuja mara moja.

Bila malipo ya ziada. Kwa kutumia bajeti ya jiji inayotokana na kodi tu.

Kama mji hauna huduma hii, tusijishebedue kufananisha maisha ya Dar na Ulaya.
 
Umenikumbusha story ya demu wa Uswahilini aliyeenda ushuani akasononeka kwa kuwa mitaa iko kimya sana, hakuna ngoma, hakuna kusutana.
 
Drainage system pia ni UOZO mtupu! Mvua kidogo tu jiji lote halitamaniki kwa mafuriko.
 
Umenikumbusha story ya demu wa Uswahilini aliyeenda ushuani akasononeka kwa kuwa mitaa iko kimya sana, hakuna ngoma, hakuna kusutana.
Mimi nakumbuka wakati niko O-level mwanzoni nilikuwa nakaa na masela, msosi wa kugombania fujo nyingiii.

Sasa, kuna Mkuu mmoja wa Magereza akapenda sana nikaishi kwake: Kwanza kuna kuku wa mayai, mayai kila muda, baiskeli za gia kibao nikapewa za kuendea shule.

Lakini imagine, nilikuwa sina amani moyoni just from within ( for no reason) kabisa ikabidi nirudi kwa masela🤣
 
Kama nakuona vile mapigo Haile Selassie fulani hivi, mpaka bustani zinahudumiwa na wafungwa!

Kuna mshkaji fulani kwao ilikuwa hivyo, yule mfungwa alikuwa anakula good time pale nafikiri alikuwa anaomba asihamishwe.
 
Kuanzia kijichi mpaka njia panda ya neluka shuka mpaka baharini daah ni next level kule
 
Mkuu maisha ya huko oysterbay nimeishi sana tena ktk hiyo mijumba ya kifahari ila asikwambie mtu mkuu mambo yanayotokea usiku ni hatari sana yaani hao wenye hiyo mijumba wanafuga viumbe vyakutisha
Amini mkuu hao watu wanamaagano yakishirikina
Masikini kashaamka sasa tujiandae na porojo
 

Mkuu nmekuelewa vzr bila shaka wacha maisha yaendele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…