the numb 1
JF-Expert Member
- Dec 15, 2020
- 1,562
- 2,902
- Thread starter
-
- #81
Asante kwa taarifa. Hii huduma muhimu.
Wamejitahidi.
Nilivyokuja US na kuona karibu kila kimji na kijiji kina Fire Brigade nilisikitika sana kulinganisha na Dar.
Wiki jana nilienda kwa aunt yangu Kijichi kuna mitaa fulani ya ushuani flani. Sasa nikasahau namba ya nyumba na jina la mtaa maana wana vimitaa vidogo vingi. Akawa hapatikani kwa simu, yeye alijua napakumbuka. Nilikuwa nakumbuka njia mbili, ya kutokea kwa Zombe yule askari au ya kutokea kwa Filikunjombe.
Kilichonichanganya katikati mitaani nilikutana na mbwa koko wengi kuliko watu. Yani Kijichi kuna mijibwa mingi njiani. Nikakumbuka hata kwetu pale sisi ndio wa kishua, mapaka hayakomi kuzalia kwetu ila sijawahi ona yanazaliana kwa majirani.
Conclusion niliyopata: hata mbwa koko na mapaka yanajua wapi kuna makombo yakushibisha. Wanapokula miguu ya kuku na kutafuna mifupa yote hawawezi tembelewa na mbwa koko hata siku moja.
Jamani tutafute hela hata wanyama watuheshimu.
Mkuu maisha ya huko oysterbay nimeishi sana tena ktk hiyo mijumba ya kifahari ila asikwambie mtu mkuu mambo yanayotokea usiku ni hatari sana yaani hao wenye hiyo mijumba wanafuga viumbe vyakutisha
Amini mkuu hao watu wanamaagano yakishirikina
New York City.Mkuu upo US pande gan
Umeshindwa hata kupiga picha hiyo mijengo
Michango ya waumini ina nguvu sana
Mbuzi nyingine zimepigwa minyororo ya moto, sio kamba tu
Duh....kweli haya maisha hayako fear...
Ndio maana Masanja kakimbilia hukoKondoo wanalipa sana.
Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.
Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.
Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.
Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.
Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.
Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.
Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.
Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.
Watoto wake wakakasirika sana.
Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?
Baba yao akasema ameshaamua.
Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.
Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.
Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.
Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.
Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.
Ukikipata unapata balaa.
Vuta picha umeishi maisha ya taabu zote duniani afu na pepo unaikosa kimasihara[emoji85][emoji85]
Ndio maana Masanja kakimbilia huko
Tena inazidi kukuuma ukijuwa hizo raha na maisha bora ya viongozi yanatokana na kodi unayolipa, au hela waliokwapuwa Kifisadi...
Hahahaa.Yule anazifua zitakate (laundry).[emoji2957]
Kanywe supu ya pweza uongeze ukoo. Hilo unaliweza. Mijengo waachie wenye nazo.Nipo mitaa ya osterbay kwa mbali naona mjengo wa Mo Dewji kwa mbali tena naona mjengo wa Paul Makonda kwa pemben yang naona mjengo wa makamu wa rais nikapita Bongoyo road nikakutana na mjengo anaoish mtoto wa Bakhresa kwa kwel nimesikitika sana hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya kweli haya maisha hayako fear wengin tunaish tu dunian ila kuna viumbe wengine wanaenjoy life imebidi kuingia hapa simply fresh kupata hata ka kinywaji kidogo.
PESA INAUMUHIMU MKUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU TUTAFUTE PESA JAPO AJIRA NI KIKWAZO SANA
Hivi tunafananisha maisha ya Oysterbay na Ulaya.
Dar kuna huduma za umma za kuzoa taka?
Nikiwa zangu nakimbia jogging nikifika kwenye huu mjengo huwa nautazama sn..kijichi kuna watu Wana hela banaView attachment 1815319
Maisha hayana formula, wewe pambana tu huenda kesho ikawa zamu yako
Japo siyo kazi rahisi coz Kila njia ina miiba